Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
9 Novemba 2021
Mtoto wa miaka 3 hadi 5
Maendeleo ya mtoto
Katika umri huu mtoto anakuwa anajitegemea zaidi na huanza kujua zaidi kuhusu ndugu na watoto ambao wapo nje ya familia.
Huwa na muda mwingi wa kuuliza maswali na kutaka kufahamu zaidi kuhusu vitu vinavyo mzunguka. Mwingiliano kati ya familia na wanajamii yatamtengenea mtoto tabia yake na mwendendo wa maisha yake.
Mtoto kwenye umri huu anaweza kuendesha baiskeli, kutumia mkasi, na kutofautisha kati ya mwanamke na mwanaume, huweza kujivalisha kwa namna fulani na huvua nguo wenyewe. Kuchezana watoto wengine, kukumbuka sehemu fulani ya adhidhi nakuimba wimbo.
Ukuaji wa kimota
Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kuendesha baiskeli ya magurudumu matatu, kurusha mpira mikononi na anaweza kuchora duara
Mtoto mwenye miaka minne anaweza kushuka ngazi kwa kupishanisha miguu, kudaka mpira na kujivalisha nguo mwenyewe
Mtoto mwenye miaka mitano anaweza kufunga kamba za viatu mwenyewe
Mambo ya kijamii, ufahamu, hisia na lugha
Mtoto mwenye miaka mitatu anaweza kutengeneza sentensi yenye maneno matatu, kutumia viwakilishi, kujua majina yake, pia anaweza kucheza na wenzake
Mtoto mwenye miaka minne anaweza kuongea vizuri kabisa na kueleweka, pia hucheza michezo ya vitu anavyo viwaza
Mtoto mwenye miaka mitano anaweza kuandika jina lake la kwanza, kucheza kwa kushirikiana na wenzake, kuelewa na kuzifuata sheria
Mambo ya kuzingatia
Mambo muhimu ya kufanya kama mlezi wa mtoto
Endelea kusoma hadhidhi au vitabu vya watoto kwa mtoto,ili kumfanya apende kusoma na kupata maarifa
Mwache aanze kukusaidia kufanya kazi za nyumbani(baadhi ambazo anataka kuzifanya kwa usalama lakini)
Mwache mtoto acheze nawenzake na apate marafiki, mtoto ataonathamani ya wenzake na ushirikiano
Uwe makini na usizembee unapomkanya mtoto,mweleze tabia ambazo unapenda uone anafanya. Ukimwambia usifanye hiki mfuatilie uone kama anafanya ulichomwambia.
Msaidie mtoto kuongea lugha nzuri kwa kumwambia maneno yaliyokamilika nay a ki utu uzima. Mfundishe kutumia maneno sahihi na sentensi
Msaidie mtoto kupata suluhu ya shida au Matatizo yake endapo amepata Matatizo
Mruhusu mtoto afanye maamuzi madogo mfano anataka kuvaa nini, kucheza sa ngapi na kula nini
Usalama wa mtoto
Namna ya kuweka usalama wa mtoto katika umri huu
Msisitize mtoto kwanini hatakiwi kucheza barabarani na akae mbali na barabara
Uwe mwangalifu unapomruhusumtotoaendeshe baiskeli, hakikisha haingii barabarani
Hakikisha kiwanja cha mtoto kucheza hakina vitu vya hatari kama chupa zilizovunjika n.k
Mwangalie mwanao muda mwingi akiwa anacheza nje na wenzake
Hakikisha usalama wa mtoto akiwa anacheza kwenye maji, msimamie akiwa anaogelea
Mfundishe mtoto kuwa makini na watu wageni, asije ibiwa au kupewa kitu kigeni cha hatari, mfundishe kutozoeana na watu asiowajua
Wajibu wa wazazi
Ili mtoto awe na afya na akili njema ni vema mzazi
Kula na mtoto unapokuwa unakula mara nyingi iwezekanavyo. Mpatie matunda kwa wingi, mboga za majani na vyakula asilia kuliko vitu vya kusindikwa. Kunywa au kunywa vinjwaji vichache sana vyenye sukari, mafuta au chumvi kwa wingi
Mpe muda mdogo wa kuangalia TV au video au kucheza games, mpe saa 1 hadi 2 tu kwa siku ikiwa ni shule, sehemu za kulea watoto n.k
Mpe vifaa vya kuchezea vinavyoendana na umri wake kama mpira, na mpe uwanja wa kuchagua nini anataka kucheza
Elimu inayotolewa hapa ni kwa ajili ya ushauri tu na hivyo ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma makala hii.
Kwa ushauri zaidi na tiba, wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano yetu
Imeboreshwa,
9 Novemba 2021, 09:02:12
Rejea za mada hii:
CDC.CDC’s Developmental Milestones.https://www.cdc.gov/ncbddd/actearly/milestones/index.html. Imechukuliwa 03.05.2020
Medilineplus. Developmental milestone records. https://medlineplus.gov/ency/article/002002.htm. Imechukuliwa 03.05.2020
Pathways.org. 0-3month milestone. https://pathways.org/growth-development/0-3-months/milestones/.Imechukuliwa 03.05.2020
3 to 6 months: Your baby's development. Zero to Three. https://www.zerotothree.org/resources/81-3-6-months-your-baby-s-development. Imechukuliwa 03.05.2020
Positive parenting tips for healthy child development: Infants (0-1 year old). Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/ncbddd/childdevelopment/positiveparenting/infants.html. Imechukuliwa 03.05.2020