top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

​

Aina ya mazoezi ya kufanya

​

Kiukweli, mpango wa mazoezi unapaswa kuhusisha mazoezi ambayo yanaboresha uimara, nguvu, na uwezo wa kuwa mwepesi. Baadhi ya programu za mazoezi ya huruhusu sehemu mbili au zaidi ya vipengele hivi hapa chini vitumike kwa pamoja wakati huo huo wa mazoezi.

 

Mazoezi ya aerobiki

​

Neno mazoezi ya aerobiki humaanisha mazoezi ya uvumilivu na mara zote mazoezi haya hu imarisha moyo na mapafu, kwa jina jingine huitwa mazoezi ya moyo. Mazoezi haya ni muhimu katika uchaguzi wako wa mazoezi na yana faida nyingi  kiafya. Mazoezi ya aerobiki huweza kuwa pamoja na, Kuendesha baiskeli, kutembea, kukimbia, kuogelea, kucheza mpira au tenis, kucheza, mchezo wa kuteleza kwenye barafu, mchezo wa kupigana ngumi na mingine mingi jamii hii.

 

Mazoezi ya kuimarisha nguvu

​

Mazoezi ya kuimarisha nguvu ni ya umuhimu kwa afya yakiendana na mazoezi ya aerobiki, kwa jina jingine mazoezi haya huitwa mazoezi ya ukinzani. Mazoezi ya kuimarisha nguvu huweza kufanywa kwa, kuupa upinzani mwili mfano, kupiga push up,kunyanyua vitu vizito, kuchuchumaa na kuinuka, kuvuta kitu kizito. Kwa kifupi mazoezi haya hufanya misuli ya mwili ifanye kazi.

Mazoezi mazuri ya nguvu hutakiwa kuifanya misuli yote na maungio ya mwili yajongee au kufanya kazi sana. Mazoezi haya yanatakiwa kufanywa angalau mara mbili au tatu kwa wiki.

 

Mazoezi ya mjongeo

​

Mazoezi mjongeo ni mazuri kwa afya hasa kwa watu wazima kwani humarisha hali ya kufanya kazi na kutembea. Kwa watu wazima mazoezi haya ni muhimu kwani huongeza kutembea na kufanya kazi za kila siku za maisha na kuzuia kuanguka kirahisi. Lengo la mazoezi mjongeo ni kuimarisha mwendo na uwezo wa kutembea kwa kuimarisha maungio ya mwili, hasa kwenye mabega, nyonga, na mgongo. Hata hivyo, mazoezi ya pekee ya mjongeo hayahitajiki kwa watu wote, hasa wale wanaojihusisha mara kwa mara katika shughuli zinazohusisha mwendo katika maungio makubwa ya mwili viungo. Muda uliotumiwa kufanya mazoezi ya mjongeo  hauhesabiki kwenye muda wa malengo ya mazoezi ya wiki yaani dakika150 za zoezi kwa wiki.

​

Ikiwa unafanya mazoezi mjongeo, ni vema kufanya mazoezi haya wakati umetoka kufanya mazoezi ya aerobiki na ukinzani, muda huu misuli huwa ya moto na zoezi hili linaweza kufanyika vizuri. Mazoezi ya kujinyoosha ni vema kufanyika kwa taratibu na polepole na si haraka haraka.

​

Mazoezi ya kupasha mwili/Kupooza mwili

​

Mbali na mambo yaliyotajwa hapo juu, mazoezi ya wastani au ya nguvu yanafaa yakitanguliwa  au kumalizika na kitendo cha kupasha. Kupasha humaanisha kuanza na mazoezi taratibu kisha kuongeza kasi, hiii husaidia mwili kujiandaa na mazoezi makali zaidi. Kupasha baada ya mazoezi husaidia mwili kujirudia na hali ya kawaida baada ya mazoezi makali, huweza kuzuia kupoteza fahamu baada ya mazoezi.Usiache mazoezi ghafla endapo umekuwa ukifanya mazoezi ya nguvu kwani unaweza kuzimia.

​

Toleo la2

Imechapishwa12/11/2018

aerobic
mazoezi ya Kuimarishanguvu
Mjongeo
Kupasha

Sehemu hii imezungumzia aina ya mazoezi ya kufanya kuimarisha mwili kwa ujumla

​

Mazoezi ya aerobiki

Mazoezi ya kuimarisha nguvu

Mazoezi mjongeo

Mazoezi ya kupasha mwili/Kupooza mwili

MAmbo ya kuzingatia usiache mazoezi

​

​

bottom of page