Kutoona hedhi
Imeandikwa na kuhaririwa na daktari wa Uly clinic
Imeandikwa 04.12.2020
​
Utangulizi
​
Tatizo hili likijulikana pia kama kutoona damu ya hedhi, kusimama kwa hedhi, amenorrhea ama amenorea, hutokea endapo mwanamke aliye kwenye umri wa kupevuka haoni siku zake za hedhi kabisa.
​
Kuna aina mbili za tatizo la amenorea ambazo ni amenorea ya baada ya kuona hedhi
Amenorea ya kuzaliwa
Ni ile inayotokea pale mwanamke anapokuwa haoni hedhi licha ya kupevuka na kufikisha umei wa miaka 14 na kuendelea. Dalili za kupevuka baadhi yake ni kuongezeka ukubwa wa matiti na kupata nywele maeneo ya siri.
Au mwanamke amefikisha miaka 16 bila kuzingatia mabadiliko ya kubalehe yaani matiti kukua na nywele za siri kuota. Wanawake chini ya asilimia 1 duniani huzaliwa na amenorea ya aina hii.
​
Amenorea baada ya kuona hedhi
​
Ni ile inayotokea kwa mwanamke ambaye tayari alikuwa anaona siku zake lakini kwa sasa haoni siku zake kwa muda zaidi ya miezi 6 ama kutoona hedhi kwa muda wa miezi mitatu mfululizo.
Ni nini hatua ya kwanza kwenye utambuzi wa tatizo la kutoona siku za hedhi?
Historia na uchunguzi wa awali wa mwili ukisaidiwa na vipimo, utapelekea kutambua ni nini haswa kilichosababisha tatizo hilo.
Maswali ya kujiuliza
​
Jiulize maswali yafuatayo kama una tatizo la kukosa hedhi ili kuweza kusaidia kufahamu kisababishi;
-
Je umejamiiana muda uliopita? (ujauzito ni jambo la awali linalosababisha tatizo hili)
-
Kama ni amenorea ya kuzaliwa, Je mabadiliko yangu ya wakati wa kubalehe yalikuwaje?
-
Je unahistoria ya ugonjwa mkali ama misongo wa mawazo, kubadili chakula ama kula chakula kinachoweza kubadili mzunguko wa hedhi, mazoezi makali au kubadilika kwa mtima wako?
-
Una au umepata mabadiliko yoyote ya kulala, kiu, hamu ya kula ama harufu ya chakula, kutapika, kichwa kuuma, mabadiliko katika uono wako, kuchoka sana ama kutokwa na maziwa kwenye chuchu-haya yanaweza kutoa majibu kwamba kunatatizo katika tezi ya pituitary ama hypothalamus
-
Je unatumia dawa za saratani ama ulikuwa unapata matibabu kwa njia ya mionzi?
-
Je unauzito wa kawaida na urefu wa kawaida? Je una mdundo wa kawaida wa mishipa ya damu ama una shinikizo la damu la kawaida?
-
Je kuna ushahidi wa kiwango kidogo cha homoni ya estrogeni ama kuota nywele kama mwanaume?
-
Je via vyako vya uzazi vipo sawa ama vinaonyesha sababu za tatizo hili?
Nini huweza kusababisha tatizo la amenorea?
​
Sababu za asilia
Sababu hizo ni kama vile
​
-
Kunyonyesha. Kuwa kwenye kipindi cha kunyonyesha mtoto(hasa miezi sita ya kwanza baada ya kujifungua)
​
Matumizi ya dawa
​
Kama kwenye makundi yafuatayo:
-
Dawa za uzazi wa mpango au kama umetokakuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango
-
Dawa za Antisaikotiki
-
Dawa za Kutibu saratani
-
Dawa za Antidiprizanti
-
Dawa za Kutibu presha ya kupanda
-
Dawa za kutibu au kuondoa mzio(aleji)
​
Mabadiliko katika maisha
​
-
Kupungua uzito sana zaidi ya kilo kumi kutoka kwenye uzito wako wa awali
-
Matatizo ya kutokula vema
-
Kufanya mazoezi makali kupita kaisi
​
Mabadiliko ya homoni
​
Huweza kuletwa na magonjwa kama vile
-
Ugonjwa wa sindromu ya polisistiki ovari
-
Madhaifu ya tezi thairoidi
-
Saratani ya tezi pituitari
-
Kukoma kwa hedhi kabla ya muda wake
​
Madhaifu ya maumbile
​
-
Kufanyika kwa makovu kwenye kuta za ndani za mfuko wa uzazi- huweza kutokea kwenye ugonjwa wa sindromu ya ashaman- hii husababishwa na kutoa mimba au kusafishwa kwa kukwanguliwa kizazi au kufuatia matibabu ya fibroid.
-
Kutokuwa na via vya uzazi kama tatizo la madhaifu ya muleriani ambapo mwanamke anazaliwa bila kuwa na mfuko wa uzazi
-
Madhaifu ya uke- kuziba kwa uke kutokana na kuwa bikra au sababu zingine mfano uvimbe uliyo kwenye shingo ya uzazi inaweza kusababisha tatizo hili la amenorea.
​
Vihatarishi
​
Vihatarishi vya kupata tatizo hili ni pamoja na;
-
Historia katika familia ya mtu mwenye tatizo hili
-
Ugonjwa wa madhaifu ya kula
-
Kufanya mazoezi ya makali ya mwili kama riadha
Madhara ya amenorea
​
-
Kuvunjika mifupa kirahisi. Endapo imetokanana kuzalishwa kwa homoni kidogo ya estrojeni
Je ni vipimo gani vya awali vya tatizo hili?
Kipimo cha kutambua utendaji kazi wa tezi ya thairoid
​
Kipimo hiki kitatambua ama kusema kwamba tatizo hili halitokani na udhaifu katika tezi hii.
​
Wagonjwa wenye kiwango cha chini cha homoni ya thyroid hurudi katika mzunguko wa hedhi mara baada ya kupewa homoni hii kwa mfumo wa vidonge.
Kipimo cha kupima kichochezi cha uzalishaji maziwa yaani prolactine
Kipimo hiki kinaweza kutoa uhakiki ama kusema kwamba tatizo halitokani na uzalishwaji mwingi wa homoni prolactine kwa sababu asilimia 10 hadi 20 ya wagonjwa wenye tatizo hili hutokea kwa watu wenye uzalishaji mwingi wa homoni hii- kiwango kikubwa cha homoni hii kinaweza kutokea hatakama maziwa hayazalishi
Kipimo cha kupewa homoni ya progesterone- zilizopo kwenye dawa za uzazi wa mpango
Kipimo kikiwa chanya (mwanamke kuona matone ya damu) ndani ya siku mbili ama 7 baada ya kupewa dawa hii basi inamaanisha kwamba kiwango cha uzalishaji homoni estrogeni ni kikubwa kinachozidi 40pg/ml na hivyo inamaanisha tena ya kwamba tezi ya pituitari inazalisha kama kawaida kiwango cha FSH na LH na kuta za uzazi zinafanya kazi. Ikiwa kazi za homoni thairoid na prolactine zipo kawaida basi tatizo linakuwa ni kutozalishwa kwa yai kiwandani yani anovulatori
Ikiwa kipimo ni hasi (yaani mwanamke haoni siku zake basi tatizo lipo kwenye njia za utoaji hedhi kama vile ugonjwa wa asherman’s sindromu, kusinyaa na makovu kutokana na ugonjwa wa michomo katkika kuta za uzazi (husababishwa na maambukizi ya bakiteria), kuziba kwa mlango wa uzazi ama kuwa na njia ndogo, kutotengenezwa kwa via vya uzazi kabisa, kuwa na kiwango cha chini cha estrogen na ubikra.
Kipimo cha FSH na LH
Kama kipimo cha prolactin na tharoid kipo sawa na kipimo cha prolactin kipo hasi basi kipimo hiki kitafanyika ili kuweza kutambua kama tatizo la uzalishwaji mdogo wa estrogeni unatokana na kushindwa kufanya kazi kwa mzunguko wa tezi pituitari na kiwanda cha mayai(ovari)
​
-
Kiwango cha FSH kikiwa kidogo basi inamaanisha tatizo hili linasababishwa na tezi ya hypothalamus
-
Kiwango kikubwa cha FSH
​
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya.
​
​
Imeboreshwa 08.05/2023
​
Rejea za mada hii
​
-
Ulyclinic maswali na majibu kwa wateja
-
Amenorrhea. Pubmed. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/5885258/. Imechukuliwa 04.06.2020
-
Welt CK, et al. Etiology, diagnosis and treatment of secondary amenorrhea. http://www.uptodate.com/home.Imechukuliwa 04.06.2020
-
Welt CK, et al. Etiology, diagnosis and treatment of primary amenorrhea. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.06.2020
-
Bope ET, et al. Conn's Current Therapy. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2013. http://www.clinicalkey.com.Imechukuliwa 04.06.2020
-
DeCherney AH, et al. Current Diagnosis & Treatment Obstetrics & Gynecology.11th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2013. http://www.accessmedicine.com/resourceTOC.aspx?resourceID=788. Accessed Jan. 21, 2014.
-
Klein DA, et al. Amenorrhea: An approach to diagnosis and management. American Family Physician. 2013;87:781.
-
Goldman L, et al. Goldman's Cecil Medicine. 24th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2012. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.06.2020