Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Lugonda M, MD
1 Agosti 2020, 15:51:54
Anatomia ya Jicho
Ni ogani muhimu kwenye mwili ambayo humsaidia binadamu kuona vituvinavyomzunguka pamoja na kumfanya awe wima wakati wa kutembea.
Jicho limegawanyika katika sehemu kuu ambazo ni;
Sehemu ya ulinzi
Sehemu ya optiko
Sehemu ya mfumo wa neva
Sehemu ya ulinzi
Sehemu hii ya jicho hutumika katika kulinda sehemu za ndani za jicho
Obiti
Ni sehemu ya mfupa wa fuvu la kichwa, imetengenezwa na tundu la mduara ambapo jicho hukaa katika tundu hilo. Shimo hili hulinda jicho na huwa ni nyumba ya jicho
Kifuniko Jicho (Eye lid)
Ni sehemu nyembamba ya ngozi yenye misuli na tishu ambayo hulinda sehemu laini za jicho
Sclera
Ni tabaka ambalo hutumika kwa ajili ya misuli ya jicho kujishikiza ,Tabaka hili hulinda sehemu za ndani za jicho
Konjaktiva
Ni sehemu nyembamba yenye ute ute ambayo imezunguka sehemu ya nyuma ya Kifuniko jicho na sehemu ya mbele ya sclera
Sehemu za Optical (Za kuona )
Sehemu hizi hutumika katika kuona
Konea
Ni sehemu ya jicho ambayo imeambatana na sclera kwa mbele , sehemu hii huruhusu mwanga kuingia kwenye macho.
Irisi
Ni sehemu ya mduara ya jicho ambayo huonekana nyeusi , sehemu hii ina misuli laini ambayo hudhibiti pupili.
Pupil
Hii ni sehemu ya katikati ya irisi ambayo huwa na rangi nyeusi,kahawia au nyeusi.Rangi hii hutofautiana kwa mtu na mtu
Lensi
Ni sehemu ambayo ina lenzi ya mbonyeo ambayo imejishikiza kwenye misuli ya ndani ya jicho,sehemu hii ya jicho hutumika katika kutazama vitu vya karibu na mbali
Aquous na Vitreous Humour
Ni maji maji mazito yanayozunguka sehemu za mbele za irisi na sehemu za nyuma za konea ,maji maji haya huruhusu mwanga kupita bila shida yeyote
Sehemu za mfumo wa neva
Retina
Ni sehemu nyembamba yenye matabaka mengi ya tishu. Retina hupokea mwanga kutoka sehemu ya mbele ya macho na kubadilisha kuwa umeme ambayo husafirishwa kwenye neva optiki mpaka kwenye koteksi ya uono ili upate kutafsiriwa.
Neva optiki
Ni sehemu ambayo hutumika kusafirisha taarifa kutoka kwenye retina kwenda kwenye sehemu ya ubongo ambayo inatumika kutafsri picha
Koteksi ya uono
Sehemu hii hutumika kutafsiri picha zote kutoka kwenye retina
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021, 10:50:42
Rejea za makala hii,
MedicineNet.EyeAnatomy.https://www.medicinenet.com/image-collection/eye_anatomy_detail_picture/picture.htm . Imechukuliwa 1/8/2020
WebMd.EyeAnatomy.https://www.webmd.com/eye-health/picture-of-the-eyes. Imechukuliwa 1/8/2020
Glaucoma.EyeAnatomy.https://www.glaucoma.org/glaucoma/anatomy-of-the-eye.php. Imechukuliwa 1/8/2020