top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

12 Julai 2020, 18:54:01

Anatomia ya Moyo
Anatomia ya Moyo
Anatomia ya Moyo

Anatomia ya Moyo

Ni ogani ambayo inatumika katika kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili . Moyo husukuma damu kwenda maeneo mbalimbali ya mwili kwa kutumia mtandao wa mishipa mbalimbali ya damu inayoitwa ateri na Veini. Kwenye picha zilizo kwenye makal hii hapo juu, arteri zimewekwakwa rangi nyekundu na veini kwa rangi ya bluu, isipokuwa mishipa ya inayopeleka damu na kuchukua kwenye mapafu, arteri huwa na rangi ya blue na vein huw ana rangi nyekundu


Vyumba vya moyo


Moyo umegawanyika katika vyumba vikuu vinne ambavyo viwili vipo juu na viwili vipo chini, vyumba hivi vya juu na chini huwa na mawasiliano, damu hutoka kwenye vyumba vya juu kwenda vyumba vya chini. Angalia kwenye picha kwa uelewa zaidi.


Vyumba vya juu huitwa atrium ambavyo vipo viwili upande wa kushoto na kulia


Vyumba vya chini huitwa ventriko ambavyo vipo viwili upande wa kushoto na kulia


Atriamu na ventriko


Atrium ya kulia: Chumba hiki hupokea damu ambayo haina oksijeni ambayo inatoka kwenye vein kubwa ambazo ni Vena kava ya juu na chini na husukuma damu kupitia valvu ya tricuspid kwenda ventriko ya kulia


Atrium ya kushoto: Chumba hiki hupokea damu yenye oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuisukuma kupitia valvu ya maitro kwenda kwenye ventriko ya kushoto


Ventriko ya kulia: Chumba hiki husukuma damu kupitia valvu ya palmonari kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kupata oksijeni


Ventriko ya kushoto: Chumba hiki hupokea damu yenye oksijeni kupitia valvu ya aortiki kwenda kwenye aorta ambapo husukumwa kwenda sehemu mbalimbali za mwili.


Valvu za moyo


Hizi hufanya kazi za kutenganisha atria na ventriko pamoja na mishipa mingine mikubwa ya damu

Valvu zipo kwenye makundi makuu mawili ambayo ni;


  • Atrioventrikula Valvu

  • Semiluna Valvu


Atrioventrikula valvu

Hizi valvu huzuia damu isirudi kutoka kwenye ventriko kwenda kwenye atrium. Atrioventrikula Valvu ina valvu aina mbili za valvu kama ambazo ni;


Valvu ya Trikaspidi: Ni valvu iliyopo kati ya vyumba vya kulia vya atrium na ventriko

Valvu ya Bikaspid: Ni valvu iliyopo kati ya vyumba vya kushoto vya atrium na ventriko


Semiluna Valvu

Hizi valvu huzuia damu isirudi kutoka kwenye mishipa mikubwa ya moyo ya damu kurudi kwenda kwenye ventriko. Kuna aina mbili ya valvu za semiluna ambazo ni;


Valvu ya pulmonari semiluna: Ni valvu iliyopo kati ya chumba cha Ventriko na njia ya kuelekea kwenye mapafu


Valvu ya aortiki semiluna: Ni valvu iliyopo kati ya chumba cha kushoto cha ventriko na njia ya kuelekea kwenye aorta

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.

Imeboreshwa,

25 Septemba 2021, 10:51:15

Rejea za makala hii,

  1. HealthBlog.Heart.https://healthblog.uofmhealth.org/heart-health/anatomy-of-a-human-heart?amp. Imechukuliwa 10/7/2020

  2. WebMd.Heart.https://www.webmd.com/heart/picture-of-the-heart. Imechukuliwa 10/7/2020

  3. Kenhub.HeartAnatomy.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/heart. Imechukuliwa 10/7/2020

  4. MedicalNewToday.HeartAnatomy.https://www.medicalnewstoday.com/articles/320565. Imechukuliwa 10/7/202o

bottom of page