Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Lugonda M, MD
31 Julai 2020, 09:41:50
Anatomia ya Sikio
Ni ogani muhimu mwilini yenye kaziya kufanya mtu asikie sauti na piakufanya mtu awe wima (asiyumbe) wakatiwa kutembea.
Sehemu ya sikio
Sikio limegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni :
Sikio la nje
Sikio la kati
Sikio la ndani
Sikio la nje
Sikio la nje limegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo ;
Pina/auriko
Hii ni sehemu ya nje ambayo hutumika kukusanya sauti kwa ajili ya kusafirishwa kwenda sikio la kati. Sehemu hii watu wengi hutoboa na kuweka vidani na herein.
Mfereji wa sikio la nje
Mrija huu hutumika kusafirisha mawimbi ya sauti yaliyokusanywa na pina na kuyapeleka kwenye ngoma ya sikio
Sikio la kati
Sikio la kati limegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo :
Ngoma ya sikio
Ni ukuta mwembamba wenye umbo la duara ambao hutenganisha sikio la nje na la ndani. Kazi yake hutumika kukuza sauti baada ya kupokea kutoka sikio la nje.
Osiko
hujumuisha mifupa midogo mitatu ambayo hutumika kusafirisha sauti kwenda sikio la ndani. Mifupa hii muhimu ni Malleus, Incus na stapes, licha ya kuwa na kazi ya kusafirisha sauti, hufanya kazi ya kukuza mawimbi ya sauti kutoka kwenye ngoma ya sikio na kuyapeleka kwenye sikio la ndani
Mrija wa Eustachian
Mrija huu hutumika kuunganisha sikio la ndani na sehumu ya nyuma ya pua ,Mrija huu hutumika kusawazisha shinikizo ndani ya sikio la kati na kusafirisha vyema mawimbi ya sauti ,sehemu hii imezungukwa na ute ute kama ilivyo kwenye koromeo na pua
Sikio la ndani
Sehemu hii imegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo;
Koklea
Vestibula
Mifereji ya semisakula
Koklea
Ni mfupa wenye uwazi katikati na umbo la mduara na neva nyingi ambao hufanya kazi kubwa katika kusikia.
Vestibula
Hufanya kazi kubwa ya kuweka mwili wima wakati wa kutembea. Husababisha usiyumbeyumbe kama mlevi wakati wa kutembea.
Mifereji ya Semisakula
Ni mifupa yeney mirija kwa ndani yenye maji ambayo yana risepta za kutambua pozi la mwili wakati wa kutembea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021, 10:50:53
Rejea za makala hii,
AnatomyAndPhysiology.Ear.https://www.stanfordchildrens.org/en/topic/default?id=anatomy-and-physiology-of-the-ear-90-P02025 . Imechukuliwa 31/7/2020
Medscape.EarAnatomy.https://emedicine.medscape.com/article/1948907-overview . Imechukuliwa 31/7/2020
Kenhub.EarAnatomy.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/the-ear . Imechukuliwa 31/7/2020
TeachMeAnatomy.Ear.https://teachmeanatomy.info/head/organs/ear/ . Imechukuliwa 31/7/2020