Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Mangwella A, MD
16 Januari 2021, 08:04:06
Anatomia ya Ulimi
Ulimi ni kiungo cha mwili kinachohusika katika kuhisi ladha ya chakula na pia kufanya mtu aweze kuumba maneno na kuyatamka, kiungo hiki huanza kuumbwa siku ya 23 kwa kijusi aliye tumboni mwa mama.
Ulimi umeundwa na misuli mbalimbali ifikayo nane, misuli hiyo juu yake imefunikwa kwa ukuta wenye rangi ya pinki uitwao mucosal ambao huupa ulimi rangi yake ya asili. Hata hivyo pia ukuta huu huwa na vinyweleo vingi vidodo vidogo vinavyoitwa papilla ambavyo huwa na chembe zenye uwezo wa kuhisi ladha ya kile unachokitia mdomoni.
Aina za Papilla
Papilla zipo za aina mbalimbali ambazo ni; (angalia kwenye picha kwa uelewa zaidi)
Filiform
Fungiform
Foliate
Circumvallate au vallate papilla
Ulimi umejishikiza nyuma ya kinywa na kwenye mfupa wa hyoid kwa kutumia tishu ngumu, upande wa mbele vivyo hivyo umeshikizwa na tishu ngumu yenye jina la frenum.
Ulimi pia huwa na mishipa mingi ya fahamu yenye kazi ya kusafirisha hisia za ladha kwenda na kurudi baina ya ulimi na mfumo wa kati wa fahamu. Sehemu yoyote ya ulimi inaweza kuhisi ladha yoyote ile ya chakula.
Kazi ya ulimi
Kazi kuu ya ulimi ni kuhisi radha, kusaidia kumeza chakula na kuumba maneno. Ladha zinazoweza kuhisiwa na ulimi ni za aina tano ambazo ni;
Ladha ya uchungu
Ladha ya utamu
Ladha ya chumvi
Ladha ya uchachu
Ladha ya ummami
Kitiba ulimi huwa kiungo muhimu sana katika kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili, baadhi ya magonjwa yanayoweza kuangalia kwa kuangalia ulimi ni kama vile;
Upungufu wa virutubisho mbalimbali mfano upungufu wa madini chuma, folate na vitamin B12 deficiency
Tatizo la Glossitis
Upungufu wa homoni ya estrogen
Ugonjwa wa UKIMWI na maambukizi ya Kirusi cha EBV
Magonjwa ya zinaa kama kaswende
Ugonjwa wa Crohn's na Ulcerative Colitis
Sindromu ya Behcet's
Pemphigus
Maambukizi ya kirusi cha herpes simplex
Ugonjwa wa histoplasmosis
Ugonjwa wa reactive arthritis (au sindromu ya Reiter's)
Utapiamlo
Saratani mbalimbali na
Magonjwa mengine mengi
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021, 10:49:18
Rejea za makala hii,
Fact-or-fiction-the-tongue-is-the-strongest-muscle-in-the-body. https://www.scientificamerican.com/article/fact-or-fiction-the-tongue-is-the-strongest-muscle-in-the-body/#. Imechukuliwa 16.01.2021
Tongue. https://stanfordmedicine25.stanford.edu/the25/tongue.html. Imechukuliwa 16.01.2021
Charles M. Huguley, JR. The Tongue. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK236/. Imechukuliwa 16.01.2021
Tongue diagnosis. https://www.nhp.gov.in/UploadFiles/microsite/635846561062513669_1.pdf. Imechukuliwa 16.01.2021
BRIAN V. REAMY etal. Common tongue conditions in primary care. https://www.aafp.org/afp/2010/0301/p627.html. Imechukuliwa 16.01.2021