Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sima A, CO, Dkt. Benjamin L, MD
27 Oktoba 2020, 08:15:22
Mifupa ya kifua (Mbavu)
Kuna jumla ya mifupa 12 ambayo inatengeneza kifua, Mifupa hii imeungana na uti wa mgongo kwa nyuma na mbele imeunganishwa na kifua kupitia cartilage
Makundi ya mbavu
Mifupa ya Mbavu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni:
Mbavu halisi
Mbavu isiyo halisi
Mbavu halisi:
Ni mifupa ambayo inayo kichwa, shingo na mwili
Kichwa: Ni sehemu ambayo inaungana na uti wa mgongo inayo umbo la mduara lenye vifundo fundo
Shingo: Ni sehemu ambayo haina mnyanyuko, huunganisha kichwa na mwili wa mbavu
Mwili wa mbavu: Ni sehemu ambayo ipo tambarale na yenye mfumo wa neva na mishipa ya damu. Hutumika katika kulinda neva hizo pamoja na mishipa ya damu
Mbavu isiyo halisi
Huhusisha mbavu namba 1,2,10,11 na 12 ni mifupa ambayo huelezeka kama mifupa ambayo siyo halisi kwa kukosa sifa mojawapo ya kuwa na kichwa, shingo au mwili
Mbavu ya kwanza:
Mbavu hii huwa fupi na pana kuliko mbavu zingine na pia hii imepitiwa na mshipa mkubwa wa damu wa subclavian
Mbavu ya 2:
Mbavu hii ni nyembamba na ndefu kuliko mbavu ya 1, mbavu hii hushikiria misuli ya serratus
Mbavu ya 10:
Mbavu hii ina facet moja ambayo huifanya kuungana na uti wa mgongo
Mbavu ya 11 na 12:
Mbavu hii haina shingo na inayo facet moja tu ambayo huifanya kuungana na mifupa ya uti wa mgongo
Mifupa yote 12 ya mbavu inaungana kwa nyuma na mifupa ya uti wa mgongo na kutengeneza jointi ambazo ni:
Jointi ya Kostotransvesi: Ni jointi kati ya mbavu na uti wa mgongo
Jointi ya Kostovetebro: Ni jointi kati ya kichwa cha mbavu kwa juu na sehemu ya chini ya mifupa uti wa mgongo
Kwa mbele mifupa imeungana na sehemu zifuatazo ambazo ni :
Mbavu ya kwanza na ya pili: Mbavu hizi zimeungana kwa mbele na mfupa sternum
Mbavu ya 8 na 10: Mbavu hizi zimeungana na cartilage kwa sehemu ya juu
Mbavu ya 11 na 12: Mbavu hizi zimeungana Pamoja sehemu ya mbele na huwa chini ya kifua yaani sehemu ya tumbo
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021, 10:49:58
Rejea za makala hii,
TeachMeAnatomy.RibsAnatomy.https://teachmeanatomy.info/thorax/bones/ribcage/. Imechukuliwa 6/10/2020
Kenhub.RibsAnatomy.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/the-ribs. Imechukuliwa 6/10/2020
Britanica.RibsAnatomy.https://www.britannica.com/science/rib-cage. Imechukuliwa 6/10/2020
RegisteredNurse.RibsAnatomy.https://www.registerednursern.com/ribs-anatomy/. Imechukuliwa 6/10/2020