top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. David A, MD

27 Oktoba 2020, 10:30:38

Mifupa ya Mkono
Mifupa ya Mkono
Mifupa ya Mkono

Mifupa ya Mkono

Mkono umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni sehemu ya juu ya mkono ambayo ipo katikati ya bega na kiwiko, sehemu ya kati ya mkono ambayo ipo katikati ya kiwiko na jointi za viganjani na sehemu ya mwisho ni kiganja cha mkono. Tazama picha kwa kuelewa zaidi


Sehemu ya juu


Sehemu ya juu ya mkono inayo mfupa uitwao humeraz


Humeras: Huu ni mfupa uliopo sehemu ya juu ya mkono ambao katika sehemu yake ya juu una kichwa cha humerus ambacho kinaunganisha mkono na tundu la glenoid kwenye scapula na huwa na ramani zifuatazo;


  • Shingo ya humeraz: Sehemu ipo pembeni juu kwenye mfupa huu wa humeraz

  • Tyubako kubwa na ndogo: Hizi ni sehemu zilizopo juu kwenye humerus ambazo hutumika kama vishikizo vya misuli mingine

  • Epikondaili ya kati: Ni sehemu ya mfupa iliyoinuka na kuingia kwa ndani. Hutumika kama kishikizo cha misuli kutoka sehemu zingine za mkono

  • Epikondaili ya pembeni: Ni sehemu ya mfupa iliyoinuka ambayo ipo pembeni ya mfupa wa chini wa humerus. Hutumika kama kishikizo cha misuli kutoka sehemu zingine za mkono

  • Troklea: Ni mfupa uliopo chini kwenye humeraz ambao hutumika kama kiunganishi na mifupa ya ulna na radiaz kwenye sehemu ya kati ya mkono

  • Capitulum: Ni mfupa uliopo pembeni ya trochlea ambao hutumika kama kishikizo na mifupa mingine kwenye mkono


Sehemu ya kati


Sehemu ya kati ya mifupa imetengenezwa kwa mfuwa wenye jina la radiaz na alna


Alna:

Mfupa huu upo karibu na mfupa wa radiaz ambao upo pamoja kama mifupa ya sehemu ya kati ya mkono. Mfupa huu upo kwa ndani ulinganisha na radiaz. Mfupa huu huungana na radiaz kupitia jointi inayoitwa radioalna


Radiaz:

Mfupa huu upo karibu na mfupa wa alna ambao upo pamoja kama mifupa ya kati ya mkono. Mfupa huu upo pembeni ukilinganisha na ulna. Mfupa huu una kichwa chake ambacho huunda sehemu ya juu ya mfupa ,kichwa cha radius huungana ulna kutengeneza jointi ya radioalna. Sehemu ya chini ya radiaz huungana na mifupa ya viganjani ambayo inajulikana kama Kapo na hivyo hutengeneza jointi iitwayo radiokapo.


Kiganja


Sehemu ya viganjani imetengenezwa kwa mifupa Ifuatayo:


Mifupa ya Kapo:

Ni mifupa midogo midogo ambayo huunda vigaja vya mkono. Jumla ya mifupa hii ipo 8. Mifupa hii imejipanga katika safu kuu mbili ambapo safu ya juu ni mifupa 4 na safu ya chini ni mifupa 4. Mifupa iliyopo kwenye safu ya juu ni scaphoid, lunate, triquetrum na pisiform. Mifupa iliyopo kwenye safu ya chini ni trapezium,trapezoid ,capitate na hamate


Mifupa ya metakapo:

Hii ni mifupa ambayo huunda Sehemu ya mkono ambayo hutumika kupigia makofi. Mifupa hii ipo jumla ya 5.Mifupa hii ipo kati ya mifupa ya Kapo na ile inayounda vidole ambayo ni Falenks .Sehemu ya juu ya Metakapo huungana na sehemu ya chini ya mifupa kapo kutengeneza jointi ya Metakapofalenks na sehemu ya chini ya meatakapo huungana na sehemu ya juu ya falenks kutengeneza jointi ya metakapofalinjo


Kidole gumba na vidole vingine huundwa na sehemu ya mifupa inayoitwa falenks, jumla ya mifupa inayounda vidole pamoja na kidole gumba ni mifupa 14


Mifupa hii hushikiliwa na ligamenti Pamoja na misuli mbalimbali kwenye mikono na huisaidia kufanya kazi vyema

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.

Imeboreshwa,

25 Septemba 2021, 10:51:58

Rejea za makala hii,

  1. UpperLimbBone.Opentext.https://opentextbc.ca/anatomyandphysiology/chapter/8-2-bones-of-the-upper-limb/. Imechukuliwa 1/10/2020

  2. UpperLimbBone.TeachMeAnatomy.https://teachmeanatomy.info/upper-limb/bones/. Imechukuliwa 1/10/2020

  3. UpperLimbBone.Getbodysmart.https://www.getbodysmart.com/upper-limb-bones. Imechukuliwa 1/10/2020

  4. UpperLimbBone.KenHub.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/upper-extremity-anatomy. Imechukuliwa 1/10/2020

bottom of page