Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Ang’zayati
Ang’zayat ni neno la Kiswahili lililotokanana neno la kizungu “anxiety” lililotokana na neno la kiratini anxus likiwa linamaanisha shauku kuu, hofu kuu ya nini kitakachotokea.
Ang’zayati inaweza kuwa ni hali ya kawaida kwa binadamu, na wakati mwingine inaweza ikawa ni ugonjwa wa akili, huweza kusababishwa na msongo wa mawazo, madawa ya kuchangamsha mwili kama amphetamine, kahawa, kokaine, bangi na mengine mengi na madhara ya kuacha dawa hizo, madhaifu ya mfumo wa fahamu, (kama yanayotokana na majeraha ya ubongo, maambukizi, madhaifu ya mfumo wa ndani wa sikio), madhaifu kwenye mfumo wa kadiovasikula(kufeli kwa moyo, arizimiazi) madhaifu ya mfumo wa endokrein(kuzalishwa kwa wingi homoni za thairoidi, adreno, upungufu wa sukari kwenye damu, feokromosaitoma) au kugazilika kwa mfumo wa upumuaji kutokana na pumu, ugonjwa wa mapafu wa COPD
Siku zote muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote
Imeboreshwa 10.03.2020
Rejea
-
Ulyclinic