top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

Anjaina pektoris

Anjaina ni neno la kiswahili lililotokana na neno la kiingereza angina,hili nalo lililotokana na neno la kilatini angere, lenye maana ya kugandamiza, na neno pektoris limetokana na neno la kiigereza pectoris  ambalo limetokana na neno la kilatini pectus linalomaanisha kifua, hivyo Anjaina pektoris hutumika kwenye kumaanisha hisia za maumivu ya mgandamizo wa kifua, kubana kwa kifua au hisia za kunyonga kifuani.

 

Maumivu haya hutokea kwa sababu ya kukosa damu kwenye maeneo Fulani la moyo kutokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya arteri.

Kwa uelewa soma Zaidi kuhusu maumivu ya kifua bonyeza hapa

Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii

Imeboreshwa 10.03.2020

 

Rejea

  1. Ulyclinic

  2. Dictionary.com imechukuliwa tarehe 2.10.2019

bottom of page