Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
Anozmia
Anozmia ni neno kiswahili lililotokana na neno la kiingereza anosmia ambalo lilitoholewa kutoka neno la kigiriki “osme” lenye maana na nusa na “an” linaloanza ni neno la kizungu linalomaanisha “bila” hivyo neno anozmia linatumika kumaanisa kupoteza uwezo wa kunusa au kutokuwa na uwezo wa kunusa
Baadhi ya maneo mengine yanayotumika ni kama upofu wa kunusa
Anozmia mara zote husababishwa na kuziba kwa tezi za kunusa kutokana na
-
Homa mafua(mafua ya virusi)
-
Rhinaitis
-
Homa ya hay
Kupoteza uwezo wa kunusa ni kawaida jinsi mtu anavyozeeka umri,, lakini kuna baadhi ya dawa zinaweza kuongeza au kuharibu uwezo wa kunusa. Sababu zingine zinazoleta tatizo hili zinatokana na kuharibika kwa mishipa ya fahamu inayopitisha taarifa za kunusa kuharibika huku huweza kutokana na kupata ajali mbaya kichwani, maambukizi ya virusi ndani ya kichwa na tiba mionzi kichwani.
Magonjwa ya mifumo ya mwili mfano ni ajali ya cerebrovasikula, ugonjwa wa Alzheimer daimenshia, kisonono, saratani ya ubongo na magonjwa ya mfumo wa tezi za endokrini, magonjwa ya lishe na magonjwa ya madhaifu ya mfumo wa fahamu.
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii
Imeboreshwa 15.11.2020
Rejea
-
Oxford English dictionary
-
Ulyclinic