Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
Ataksia
Ataksia ni neno la Kiswahili lililotoholewa hapa ULY CLINIC kutoka kwenye neno la kitiba “ataxia” ambalo lilitokana na neno la Kigiriki ataxis (a-axis) “a” inamaana bila, na “axis” ikiwa na maana ya mpangilio. Hivyo neno ataksia linatumika kitiba kumaanisha “kutembea bila mpangilio” .
Kwa ufafanuzi Zaidi ataksia humaanisha kukosa mpangilio, au kujongea pasipo mpangilio. Mtu mwenye tatizo la ataksia huwa hana mpangilio kwenye mjongeo wa miguu na mikono, ikiwa inamaanisha kukosa uwezo wa kujongea vema. Tatizo hili halitokani na udhaifu wa misuli lakini hutokana na udhaifu au shida kwenye sehemu ya ubongo iitwayo serebela, vestibula au udhaifu wa hisia za propioseptivu
Mambo au hali zinazoweza kusababisha tatizo la ataksia ni pamoja na;
-
Dawa ( mfano pombe, aminoglutethimide, anticholinergics, phenytoin, carbazepine, phenobarbital, na tricyclic antidepressants),
-
Kiharusi au kiharusi cha mpito
-
Ugonjwa wa Sklerosis
-
Jeraha kichwani
-
Magonjwa ya kurithi (ataksia ya cerebela ya kuzaliwa , ataksia ya Friendreich, ataksia ya telangiectasia)
-
Maambukizi(maambukizi ya Surua au ensefalaitis)
Aina za ataksia
Ataksia ya cerebela- hutokana na majeraha kwenye serebelamu au mishipa yake ya kutoka na kuingia kwenye pedankle ya cerebela, poni au nuklia nyekundu.
Ataksia ya vestibula- hutokana na majeraha sehemu yoyote ya mshipa wa fahamu wa fuvu namba nane unapopita kutoka kwenye labrinthi hadi kwenye shina la ubongo na kwenye nuklia ya vestibula. Nistagmasi hutokea sana kama dalili moja wapo ila huwa ni ya upande mmoja wa jicho. Ataksia aina hii huwa inategemea pia mvutano wa gravity, mtu akiwa amelala akichunguzwa ni vigumu kugundua kama anatatizo la mjongeo wa misuli ya miguu, labda akiwa anasimama na kutembea tu.
Ataksia ya sensori- huweza kutokana na majeraha sehemu yoyote kwenye mishipa inayopeleka taarifa kwenye lobu ya parieto coteksi. Uchunguzi unaweza kuonyesha madhaifu ya mahari joint ilipo, madhaifu ya mtetemo, na hisia kwenye miguu na wakati mwingine kwenye mikono, kupoteza uwezo wa kusimama wima, na kuyumba ukisimama wimba na kufumba acho(Kiashiria cha Romberg) na kuwa na slaping Geiti.
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
Rejea
-
ULY CLINIC
-
MEdical problem in dentistry na crispian scully toleo la 6
-
NINDS ataxias and cerebellar or spinocerebellar degeneration information page. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/All-Disorders/Ataxias-and-Cerebellar-or-Spinocerebellar-Degeneration-Information-Page. Imetazamwa Dec. 5, 2019.
-
Todd PK. Overview of cerebellar ataxias in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imetazamwa Dec. 5, 2019.
-
Classification of ataxia. National Ataxia Foundation. https://ataxia.org/fact-sheets/. Imetazamwa Dec. 5, 2019.
-
Ataxia telangiectasia. National Cancer Institute. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/genetics/ataxia-fact-sheet. Imetazamwa Dec. 5, 2019.