Michuboko ya konea
Michubuko kwenye konea ni michubuko inayotokea kwenye ukuta mweupe unaolinda jicho- ukuta huu upo mbele ya macho yako. Konea huweza kuathiliwa na uchafu, vumbi, mchanga, nywele, vyuma vidogodogo , lensi za kuvalishwa jichoni au hata karatasi. Michubuko inayotokana na mimea huweza kudumu kwa muda kadhaa kabla jicho halijapona kama vile inayotokana na miba ya mti wa msonobari.
Dalili na viashiria ni kama vile;
Maumivu
Kuhisi kama kuna changalawe kwenye jicho
Kutoa machozi
Kuumizwa na mwanga
Kichwa kuuma
Kama umepata michubuko kwenye jicho, tafuta matibabu sahihi. Kama michubuko isipotibiwa kwa mda,jicho linaweza kupata maambukizi na kusababisha vidonda kwenye konea.
Matibabu ya awali unayoweza kufanya baada ya kupata michubuko kwenye macho ni;
Safisha macho yako kwa maji safi au maji ya saline(maji haya huuzwa maduka ya madawa)
Tumia kikombe kiweke kwenye soketi ya jicho- juu ya mfupa wa soketi ya jicho, kisha ruhusu maji yatiririke na hivi itasaidia kuosha macho kuondoa uchafu na vitu vigeni kwenye jicho
Konyeza jicho mara nyingi-hili husaidia kuondoa vipande vidogo dogo kwenye jicho
Vuta kope ya juu ilale juu ya kope ya chini- Zoezi hili husababisha macho yako yatoe machozi kisha kama kuna uchafu unaweza kuondolewa. Pia kope ya chini huweza kusafisha ndani ya kope ya juu kwa kufanya zoezi hilo.
Fanya yafuatayo usisababishe tatizo lako kuwa baya
Usiondoe uchafu uliongangania kwenye jicho au unaosababisha ukashindwa kufunga macho
Usifikite macho yako
Usishike macho kwa pamba, au vitu vingine
Kama unatumia lensi za kuvaa kwenye macho, usivae kwa mda ili upone
Michubuko kwenye macho mara nyingi huweza kupona ndani ya masaa au siku 2.
Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Comments