top of page

Rudi nyuma

​

Imeandikwa na Daktari wa ULY CLINIC

​

Matibabu ya majeraha ya kuvilia kwa damu (bruizi)

​

A bruizi ni neno la tiba linalotumika na ULY CLINIC, neo hili lilitokana na neno la kitiba "bruise" ambalo lilitoholewa kutoka kwenye neno la kifaransa "bruiser" linalomaanisha "kupasuka" 

 

Katika tiba neno Bruizi linatumika kumaanisha kupasuka kwa mishipa midogo ya damu maeneo chini kidogo ya ngozi na kusababisha damu kuvilia na kuonyesha rangi nyeusi au ya bluu chini ya ngozi ambayo hubadilika jinsi siku zinavyoenda.

 

Ni nini husababisha bruizi?

​

  • Majeraha ya michezo, hutokana na mgandamizo, mikraruzo au kuteguka kwa viungo vya mwili, mara nyingi huambatana na uvimbe na huweza kutokea pia kutokana na kutumika sana kwa kiungo cha mwili

 

  • Konkasheni- ni majeraha ya wastani kwenye ubongo, hutokea baada ya kupigwa na kitu kichwani au majeraha kutokana na kusimama ghafla. Dalili zingine huweza kuwa pamoja na kuchanganyikiwa, kupoteza fahamu, kuona vitu vinazunguka, kuona ukungu machoni, kichefuchefu na kutapika, kuumizwa na mwanga

 

  • Ugonjwa wa thrombosaitopenia- huu ni ugonjwa wa upungufu wa chembe zahani za damu, ugonjwa huu hufahamika pia kama ugonjwa wa upungufu wa chembe sahani za damu. Dalili zinazoweza kuambatana na ugonjwa huu hutegemea ukubwa wa tatizo, huweza kuwa kati ya bruizi,  vidoti vidogo vyenye rangi nyekundu, zambarau au nyeusi, kutokwa na damu puani, kutokwa na damu kwenye kwenye fizi , kutokwa na damu mu da mrefu kutokana na jeraha, kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa na mkojo, kutapika damu na kupata hedhi nzito

 

  • Saratani ya damu- leukemia. Huambatana na uzalishaji wa chembe nyeupe za damu ambazo hazijakomaa au uzalishaji wa chembe nyeupe za damu zisizo za kawaida. Dalili huwa pamoja na kuvimba kwa mitoki haswa eneo la shingo na kwapa, kuvimba kwa ini na bandama, kutokwa na vidoti vya damu kwenye ngozi(vidoti vya patekio), kutokwa na damu kirahisi mfano wakati wa kupiga mswaki, kutokwa na damu muda mrefu, homa, kutetemeka mwili, kupata maambukizi ya mara kwa mara. Soma zaidi kuhusu makala hii kwa kubonyeza  “saratani ya damu

  • Majeraha kichwani- kutokana na kugonjwa au kugongesha kichwa kwenye kitu

  • Kuteguka katika maungio. mfano mkono au mguu

  • Mijongeo ya misuli au kugandamizwa kwa misuli- hutokana na kutumia isivyo kawaida kwa misuli au kugonjwa na kitu

  • Magonjwa mengine ya upungufu wa vigandisha damu kama huleta dalili za kuvilia kwa damu kwenye maungio ya mwili, tumbo, misuli na chini ya ngozi

  • Ugonjwa wa von willebrand- upungufu wa VWF

  • Ugonjwa wa hemophilia A- hutokana na kukosa kwa vigandisha damu namba VIII, IX, or XI.

  • Ugonjwa wa hemophilia B- hutokana na kuzalishwa kidogo au kukosekana na kigandisha damu namba IX-

  • Upungufu wa kigandisha damu namba X- kwa jina jingine huitwa upunguwa wa kigandisha damu cha Stuart-Prower

  • Upungufu wa kigandisha damu namba V, II

  • Ugonjwa wa varikosi veini

  • Ugonjwa wa dipi venaz thrombosis- hutokea endapo damu imeganda chini kwenye mishipa ya damu ya ndani zaidi, dalili huweza kuwa kuvimba kwa kanyagio au kiwiko cha mguu, kuvimba kwa mguu paoja na maumivu, kubadilika rangi ya ngozi,ngozi kuwa na umoto eneo lililoathirika na kubadilika rangi kuwa kama nyekundu au bluu

  • Matumizi ya dawa mbalimbali kama aspirini, dawa za kuyeyusha damu, dawa za antibiotiki, dawa za kupeka jamii ya steroidi zinazotumika kutibu aleji na magonjwa ya ngozi, asthma na ezima

  • Uzee- unapofikia uzeeni, damu hutoka kirahisi kwa sababu ya ngozi kutoka mafuta ya kutosha katika kitako chake yanayolinda mishipa chini ya ngozi isipasuke, hii hupelekea kupata majeraja kirahisi na kuvilia kwa damu chini ya ngozi

 

Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu matibabu ya nyumbani ya bruiz yanayoshauriwa na ULYCLINIC â€‹

​

Mwone daktari kwa ushauri na uchunguzi zaidi endapo

​

  • Kuna maumivu makali kwenye eneo lenye bruizi

  • Bado unapata maumivu siku tatu baada ya kupata jeraha dogo

  • Bruzi imetokea bila sababu ya msingi

  • Una bruizi kubwa, au zinazotokea mara kwa mara, zilizo usoni au mgongoni

  • Unapata bruizi kirahisi au una historia ya kutokwa na damu kirahisi kama vile kama umekwanguliwa kidogo damu zinatoka muda mrefu kuliko mtu mwingine akiwa na jeraha kama lako.

  • Una historia ya kutokwa na damu kwenye fizi kirahisi unapopiga mswaki au  puani bila sababu.

  • Una matatizo ya kutokwa na damu.

  • Kuna historia kwenye familia ya kutokwa na damu kirahisi.

​

Dalili zilizoorodheshwa hapo juu zinaweza kumaanisha matatizo ya kutokwa na damu hivyo unahitaji ushauri zaidi kutoka kwa daktari wako​​.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba mahari popote ulipo Tanzania kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.

​

Imeboreshwa, 17.03.2020

​

Rejea za mada

​

  1. Muscle contusion (bruise). American Academy of Orthopaedic Surgeons. http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm?topic=A00341. Imechukuliwa 10.03.2020.

  2. Approach to sports injuries. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/injuries-poisoning/sports-injury/approach-to-sports-injuries. Imechukuliwa 10.03.2020.

  3. Buttaravoli P, et al. Contusion (bruise). In: Minor Emergencies. 3rd ed. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2012. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.03.2020.

  4. Kraut EH. Easy bruising. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 10.03.2020.

  5. Skin care and aging. National Institute on Aging. http://www.nia.nih.gov/health/publication/skin-care-and-aging. Imechukuliwa 28.07.2020.

  6. Muscle contusion (bruise). American Academy of Orthopaedic Surgeons. http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm?topic=A00341. Imechukuliwa 28.07.2020.

  7. Hoffman R, et al. Clinical approach to the patient with bleeding or bruising. In: Hematology: Basic Principles and Practice. 6th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2013. http://clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.07.2020

  8. Goldman L, et al., eds. Approach to the patient with bleeding and thrombosis. In: Goldman-Cecil Medicine. 25th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. http://clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.07.2020

  9. Paddock M, et al. Bleeding diatheses: Approach to the patient who bleeds or has abnormal coagulation. Primary Care: Clinics in Office Practice. 2016;43:637.

  10. Falls and fractures. National Institute on Aging. https://www.nia.nih.gov/health/publication/falls-and-fractures. Imechukuliwa 28.07.2020

Bruizi--ulyclinic
bottom of page