Imeandikwa na ULY CLINIC
​
Chanjo ya Tetenus kwa wanawake
Chanjo ya Tetenus ni chanjo inayotolewa kwa watu wote ili kujilinda na madhara ya maambukizi ya bakiteria anayeitwa clostridium teteni, bakiteria huyu anapoingia mwilini hutoa suu inayosababisha kuharibu kwa usafilishaji wa taarifa za mishipa ya fahamu ya misuli. Matokeo yake ni mtu huanza kupata dalili mbalimbali kama zilivyotajwa hapo chini. Maambukizi ya bakiteria huyu yanaweza kyutokana na
-
kukatwa na kitu chenye kutu
-
kuweka mchanga katika kidonda
-
kukwatwa na kitu chochote chenye ncha kali kilichogusana na udongo
-
wakati wa kujifungua mtoto anaweza kupata tetenus kutokana na kisu kilichotuika kukata kondo la uzazi
-
n.k
Bakiteria anayesababisha tetenus hupatikana katika sehemu zifuatazo;
-
Udongo
-
Kinyesi cha wannyama
-
Vumbi
​
Dalili za Tetenus
​
dalili za tetenus zinaweza kuonekana siku chache hadi wiki kadhaa mara baada ya tukio, dalili hizo hutokana na kuharibiwa kwa mfumo wa fahamu na hivyo huwa kaa zifuatazo
-
Kukakamaa kwa misuli ya kinywa
-
Kukakanmaa kwa misuli ya shingo
-
Kushindwa kumeza chochote
-
Kukakamaa kwa misuli ya tumbo
-
Kupata maumivu wakati misuli ya mwili inapokakamaa yenyewe, inayoweza kuamshwa na vitu vidogo kama,sauti ya mtu, mwanga ama kushikwa na mtu
Dalili zingine ni kama
​
-
Homa
-
kutokwa jasho
-
Kupanda kwa shinikizo la damu
-
Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
Wakati gani wa kupata chanjo ya tetenus
Serikali imeweka utaratibu kwa wanawake kupata chanjo bure kabisa katika vituo vya afya hasa ngazi ya wilaya(kwa nchi ya Tanzania) kwa ujumla mwanamke anatakiwa kupata chanjo tano kipindi chake cha uzazi ambazo hutolewa kama ilivyoandikwa katika jedwali hapo chini
​
​
​
​
​
Vihatarishi vya kupata tetenus
Bakteria wanaosababisha tetenus lazima wawe na njia ya kuingia mwilini ndipo wasababishe tetenus ambapo hata hivyo vihatarishi vinavyomuweka hatarini mtu kupata tetenus ni kama vile
-
Kutokupata chanjo, kutopokea chanjo inayofuata dhidi ya tetenus ama kuacha kuendeleza kupokea chanjo kama inavyotakiwa
-
Jeraha linalozama ndani ya mwili linalosababisha bakiteria wa tetenus kuingia ndani ya mwili kupitia mlango huo
-
Kuwepo kwa bakiteria wanaosababisha tetenus
-
Jeraha lolote
-
Kutobolewa na kitu kama msumali,n.k
Tetenus pia hutokea kwa watu wenye majeraha kama yafuatayo
-
Majeraa ya kujikata- kujigonga na nyundo, kujitoboa na pini ama kuchora tatuu ama kujidunga madawa ya kulevya
-
Jeraha kutokana na kupigwa risasi
-
Jeraha ya kuvunjika mifupa
-
Jeraha la kusagika kwa maungio yoyote ya mwili ama misuli, ngozi
-
Majeraha kutokana na kuungua moto
-
Majeraha ya upasuaji
-
Majeraha kutokana na kuchoma sindano
-
Maambukizi ya masikio
-
Kungatwa na wanyama
-
Vidonda visivyo visafi katika miguu
-
Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto ambacho bado hakijakauka kutoka kwa mama ambaye hajapata chanjo kama inavyotakiwa
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 9.11.2020
​
ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
​
​​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​
-
Huduma za kliniki wakati wa ujauzito
-
Namna ya Kujua tarehe ya kujifungua