Imeandikwa na mfamasia wa ULY CLINIC
Clomiphene
​
Ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la selestive Estrogen receptor modulator, dawa zingine zilizo kwenye kundi hili ni pamoja na bazedoxifene/conjugated estrogens, Clomid, clomiphene, Duavee, Evista, ospemifene, Osphena, raloxifene, Serophene na tamoxifen.
​
Dawa hii hutumika kuongeza uzalishaji wa mayai kwa wagonjwa wenye tatizo la polisistiki ovarian sindromu na wanwake wenye matatizo ya ugumba
Hupatikana kama kidonge cha miligramu 50 na 100
​
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa kwa baadhi ya watu ni pamoja na;
-
Kukua kwa ovari
-
Kutokwa na jasho
-
Mvurugiko wa hali ya tumbo
-
Kuona malengelenge
-
Kichefuchefu na kutapia
-
Mvurugiko wa hali ya titi
Maudhi mengine ambayo yalijulikana baada ya dawa kuingia sokoni ni;
Kwenye mfumo moyo na mishipa ya damu: arizmia, shinikizo la juu la damu, embolizim ya palmonari, mapigo ya moyo kwenda haraka au taratibu, thromboflebaitis, kuishiwa pumzi.
​
Ngozi: chunusi, mzio, erizima, erizima matifomi, erizima nodosa, haipatrikosis, miwasho na utikaria.
​
Mfumo wa mkojo na uzazi. Endometriosis, isti ya ovari, kukua kwa ovari, hemoreji ya ovari, ujauzito kwenye mirija ya uzazi, kupungua kwa upana wa endometria.
​
Imeboreshwa 5.03.2020
​
Rejea
BNF 78 edition 2019