top of page

Imeandikwa na daktari/Mfamasia wa ULY CLINIC

​

Dawa za kutibu tezi dume ilovimba-BPH

 

Kuvimba kwa tezi dume kwenye makala hii kunamaanisha ugonjwa wa BPH au benaini prosteti haipaplezia. BPH ni tatizo linalotokana na kukua kwa tezi dume, kukua kwa tezi hii hupelekea kuziba au kupunguza mrija wa njia ya mkojo. Tezi dume hukua jinsi mtu anavyoongezeka umri. Mwanaume anapofikia umri wa miaka 50 na kuendelea tezi dume hukua haraka sana. Katika umri huu dalili za kuvimba kwa tezi dume huanza kuonekana sana. Soma kuhusu makala ya kuvimba kwa tezi dume kwa kubonyeza hapa.

 

Dawa za kutibu tezi dume hulenga kupunguza dalili kwa kulegeza misuli ya njia ya mkojo na tezi dume, kufanyika kwa tendo hili husababisha mkojo kupita kirahisi. Dawa hizi zipo kwenye makundi mbalimbali ambayo yameorodheshwa hapa chini. Bonyeza aina ya dawa kwa maelezo zaidi.

 

Alfa bloka

 

Kundi hili ni zuri kutumika kwa wagonjwa wenye presha pamoja na tatizo la BPH

 

Mfano wa dawa kwenye kundi hili ni

  • Alfuzosin (Uroxatral)

  • Doxazosin (Cardura)

  • Prazosin (Minipress)

  • Silodosin (Rapaflo)

  • Tamsulosin (Flomax)

  • Terazosin (Hytrin)

 

5-alfa redaktaze inhibita

 

Hufanya kazi ya kuzuia uzalishwaji wa homoni(testosterone) inayofanya tezi ya prostate ikuwe , licha ya kufanya isikue, dawa hii wakati mwingine huweza kufanya tezi isinyae na hivyo mgonjwa kupata unafuu wa dalili za tezi dume.

 

Mfano wa dawa hizo ni;

 

  • Finasteride (Propecia, Proscar)

  • Dutasteride (Avodart)

 

Fosfoesteriesterazi 5 inhibita

 

Dawa kundi hili hutumika awali kutibu matatizo ya kutosimamisha uume. Hufanya kazi  hiyo kwa kulainisha misuli ya tezi ya prostate na kibofu cha mkojo. Matokeo ya matendo haya pia hupelekea  kupungua kwa dalili za tatizo la tezi dume BPH

 

Mfano wa dawa kweney kundi hili ni;

 

  • Tadalafil

  • Sildenafir

  • Vardenafil

 

Wakati mwingine dawa daktari anaweza kutumia dawa ambazo tayari zimechanganyika zaidi ya dawa moja katika matibabu mfano;

 

  • Finasteride na doxazosin

  • Dutasteride na tamsulosin

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote upate ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi. Tumia namba za simu au bonyeza pata tiba chini ya tovuti hii.

​

Rejea zamada hii

​

  1. Benign prostatic hyperplasia  treatment. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/benign-prostatic-hyperplasia/diagnosis-treatment/drc-20370093. Imechukuliwa 30.06.2020

  2. BPH treatment. Webmd. https://www.webmd.com/men/prostate-enlargement-bph/bph-choose-watchful-waiting-medication. Imechukuliwa 30.06.2020

  3. Tanzania standard treatment guidline  toleo la 2017

​

bottom of page