top of page

Ugumba kwa wanawake na wanaume-Infertility

 

Utangulizi

​

Kama kupata mimba imekuwa ni changamoto kwako na mpenzi wako, basi jua kuwa hauko peke yako na tatizo hili. Asilimia kumi hadi 15 ya wanandoa nchini Tanzania ni wagumba (tasa). Utasa huelezewa kuwa ni tatizo la  kutokuwa na uwezo wa kupata mimba licha ya kuwa unashiriki tendo la ndoa pasipo kutumia kinga au njia za uzazi wa mpango angalau kwa mwaka mmoja au baada ya miezi sita kwa baadhi ya watu.

Utasa unaweza kusababishwa na sababu moja ama nyingi zilizo kati yako wewe na mpenzi wako, au mchanganyiko wa mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuzuia mimba kutungwa au kuendelea. Kwa bahati nzuri, kuna matibabu  mengi ya usalama, ufanisi na  Msingi kwa ajili ya kukabiliana utasa-ugumba. Matibabu haya kwa kiasi kikubwa huboresha ama kurudisha nafasi yako ya kuwa mjamzito

 

Dalili za Ugumba-Utasa

 

Wapenzi wengi walio wagumba, hupata mimba ndani ya miezi sita ya kwanza ya kujaribu kutafuta mimba baada yha ushauri kutoka kwa daktari. Kwa ujumla, baada ya miezi 12 ya kujamiiana  mara kwa mara bila kinga, asilimia 90 yawanandoa hupata mimba. Wengi wa wanandoa wenye ugumba huweza kupata mimba bila matibabu yoyote

Ishara kuu ya utasa ni kukosa uwezo kwa wanandoa kupata mimba. 

Mara nyingi hakuna dalili za wazi ama za kuonekana zinazomsema mtu kuwa anaugumba

Baadhi ya wagumba  wanaweza kuwa na hedhi ya kawaida au kutokwenda hedhi kabisa. Mwanaume mgumba anaweza kupata dalili za kuharibika kwa usawia wa uzalishaji vichochezi vya uzazi (homoni) kama vile mabadiliko katika ukuaji wa nywele, mabadiliko ya kijinsia, kupungua hamu ya tendo la ndoa, au kuwa na matatizo ya umwagaji wa mbegu kwa mwanaume. Mwanaume pia  anaweza kuwa na korodani ndogo au uvimbe katika kifuko cha kutunzia mbegu.

 

Nini husababisha Utasa-Ugumba?

Ili uweze kusoma zaidi makala zetu ni lazima utumie email yako kujisajili bonyeza hapa

Utangulizi
dalili
visababishi

Sehemu hii utasoma kuhusu

​

Utangulizi

Dalili

Visababishi

Visababishi kwa mwanamke

Visababishi kwa mwanaume

Visababishi vya pamoja

Vipimo

Matibabu

​

​

bottom of page