Michomo kwenye konea
Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic
​
Utangulizi
Konea ni ukuta ulio juu(umefunika jicho) wenye umbo la kuba unayofunika sehemu ya ndani ya jicho lako. Michomo kwenye jicho husababishwa na maambukizi ya bakteria, virusi, fungasi, au vimelea. Pia michomo kwenye jicho huweza kutokea bila maambukizi , na endapo ikitokea huweza kusababishwa na majeraha madogo, kuvaa lensi za kuvaa kwenye jicho kwa muda mrefu au magonjwa mengine yasiyo ya kuambukizwa.
​
Kama jicho lako linakuwa jekundu ama unapata dalili zingine za michomo kwenye konea, kutana na daktari wako kupata tiba.
Kwa umakini na utaalamu, michomo ya kiasi kwenye jicho huweza kutibiwa vema bila kupoteza uwezo wa kuona. Kama usipotibiwa au kama maambukizi ni makali basi mtu unaweza kupoteza uwezo wa kuona maisha yako yote.
Dalili/Viashiria
-
Jicho/macho kuwa na rangi nyekundu
-
Maumivu ya jicho
-
Kutoa machozi sana ama uchafu machoni
-
Kushindwa kufungua kope za macho
-
Kuona vitu vina ukungu
-
Kupungua uweza wa kuona
-
Kuumizwa na mwanga wa kawaida wa jua-kuogopa mwanga
-
Kuhisi kuna kitu ndani ya jicho lako
Imeboreshwa mara ya mwisho 27/12/2018
​
Una email/barua pepe? ingiza email yako uendelee kusoma makala hii kuhusu kama huja bonyeza hapa kusajili moja kwa ajili yako yahoo, google mail
​
Sehemu utasoma kuhusu
​