
Kufanya CPR kwa mtu mzima
Imeandikwa na daktari wa uly clinic
Mtu mzima akizimia ghafla na akiwa hapumui ghafla angalia na sikiliza kifua chake kuona kama kifua hakichezi au hatoi sauti ya kupumua. Endapo ana dalili hizi mwambie mtu mwingine apige namba 112 kwa ajili y ambulance kuja wakati wewe unafanya CPR kama inavyoelezewa hapa chini.
-
Weka kisigino cha mkono wako kwenye kifua cha mtu unayemfanyia CPR kati ya chuchu moja na nyingine(katikati ya kifua)
-
Weka mkono mwingine juu ya mkono wako wa kwanza na uingilianishe vidole vyako
-
Kwa kutumia uzito wako wa mwili (si tu mikono yako), kandamiza kifua kwenda chini kwa umbali wa sentimita 5 hadi 6
-
Baada ya kukandamiza, mikono ikiwa kwenye kifua ruhusu kifua kijirudie kwenye hali yake ya kawaida(kama unavyo kandamiza na kuachia filimbi ili itoe sauti).
-
Rudia kugandamiza kwa kiwango cha mara 100 hadi 120 kwa dakika moja hadi msaada wa mtaalamu wa afya ufike au umechoka.
-
Kwa namna nyingine kandamiza hadi mara mbili kwa sekunde moja
Toleo la 2
Imeboreshwa 20/12/2018
Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;