top of page

22 Machi 2025, 14:56:15

Embolism ya mapafu

Embolism ya mapafu

Dalili za embolism ya mapafu ni zipi?


Dalili na ishara za embolism ya mapafu au kifungo cha mapafu hutegemea ukubwa, idadi, na eneo la vijinga vya damu vilivyokwama, lakini ni hali hatari inayoweza kusababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua.


Dalili kuu ni:

  • Kupumua kwa shida na kupumua haraka,

  • Maumivu ya kifua ya pleuriti au chini ya mfupa wa kidari,

  • Wasiwasi na mfadhaiko,

  • Mapigo ya moyo haraka,

  • Kikohozi chenye makohozi, mara nyingine chenye damu,

  • Homa ya kiwango cha chini,

  • Ngozi kuwa na rangi ya buluu), kuzimia , na uvimbe wa mishipa ya shingo (Kuvimba kwa vena jugula) ikiwa vijinga vya damu ni vikubwa,

  • Sauti za mapafu zilizotawanyika (krako ya kutawanyika) na MIruzi katika sehemu fulani iliyoathirika.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

22 Machi 2025, 14:56:15

Rejea za mada hii

bottom of page