Imeandikwa na ULY CLINIC
26 Februari 2021, 13:38:24
Kuvimba kwa ulimi
Kuvimba kwa ulimi huweza kuwa dalili ya michomo ya kinga kwenye ulimi kwa lugha ya kitiba glosaitiz.
Glosaitiz huweza kusababishwa na maambukizi, kuwasha kwa ndani au kuchoma au athari ya mzio. Kuvimba kwa ulimi pia kunaweza kusababishwa na majeraha au magonjwa kama amyloidosis.
Visababishi
Athari ya mzio, Kuvimba kwa ulimi kunaweza kutokea ikiwa una athari ya mzio kwa dawa ya meno, kusafisha sana ulimi kwa dawa, kuvaa meno bandia, kutumia mafuta ya meno, na pia kutumia baadhi ya dawa pia zinaweza kusababisha hali hii.
Ugonjwa wa Sjögren, Ugonjwa wa Sjögren husababisha uharibifu wa tezi zinazotengeneza mate. Wakati ugonjwa huu unatokea, unaweza kupata kinywa kikavu, hali inayoweza kuchochea ulimi uvimbe
Kuumia, Kuchoma au majeraha ndani ya kinywa
Upungufu wa vitamin, kiwango kidogo au cha chini cha vitamini B-12 au madini chuma kiinaweza kusababisha kuvimba kwa ulimi.
Maambukizi ya fangasi kinywani, pia inajulikana kama oral thrush, inaweza kusababisha uchochezi wa ulimi
Pombe, vyakula vyenye viungo, au tumbaku inaweza kukasirisha kinywa na kusababisha kuvimba kwa ulimi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:37:03
Rejea za mada hii