ULY CLINIC
22 Machi 2025, 15:18:47
Majeraha ya uti wa mgongo

Dalili za majeraha ya Uti wa Mgongo ni zipi?
Matumizi ya misuli ya ziada kwa kupumua hutegemea eneo na ukali wa jeraha. Jeraha chini ya L1 kwa kawaida haliathiri diaframu wala misuli ya ziada, lakini jeraha kati ya C3 na C5 huathiri misuli ya juu ya upumuaji na diaframu, na kusababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua.
Dalili na ishara zinazohusiana na majeraha ya uti wa mgongo ni:
Kuwa na rifleksi Babinski’s moja kwa moja au pande zote mbili,
Reflexi za tendoni andani zenye nguvu kupita kiasi,
Kukaza kwa misuli isivyo kawaida,
Kupoteza hisia za maumivu, joto, mkao wa mwili, au uwezo wa kutembea kwa viwango tofauti,
Sindramu Horner’s , ambayo inaweza kutokea kwa majeraha ya sehemu ya chini ya uti wa mgongo wa seviksi, na husababisha:
Kuanguka kwa kope moja,
Kupungua kwa kipenyo cha mboni ya jicho,
Kutotokwa na jasho usoni upande ulioathirika.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
22 Machi 2025, 15:18:47
Rejea za mada hii
ULY CLINIC