Imeandikwa na ULY CLINIC
20 Septemba 2021 16:13:11
Prostaitiz Kali
Prostaitiz kali ni michomo kwenye tezi dume inayotokea kama matokeo ya shambulio la mfumo wa kinga kwenye vimelea walio kwenye tezi na huambatana na dalili kali za ghafla.
Dalili
Dalili za awali huwa pamoja na;
Homa ya ghalfa
Kutetemeka
Maumivu ya chini ya mgongo
Maumivu ya misuli
Hisia za kujaa kwa kwenye periniamu
Maumivu ya maungio
Dalili zingine
Dalili zingine ni
Kukojoa mara kwa mara
Kushindwa kuzuia mkojo
Mkojo kuwa mzito
Maumivu wakati wa kukojoa
Kuziba kwa njia ya mkojo
Ishara
Tezi dume kuwa ngumu, yenye maumivu na ya moto.
Visababishi
Kisababishi kikuu cha prostaitiz kali ni maambukizi ya bakteria kwenye tezi dume, vimelea hawa mara nyingi husababisha pia maambukizi kwenye njia ya mkojo(U.T.I).
Bakteria hao hujumuisha;
Escherichia coli
Proteus mirabilis
Klebsiella species
Enterobacter species
Pseudomonas aeruginosa
Serratia species
Wapi unapata taarifa za idi kuhusu Prostaitiz kali?
Pata taarifa zaidi kuhusu prostaitiz sugu kwenye madakala za dalili na viashiria au magonjwa na saratani kwenye tovuti ya ulyclinic.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022 19:19:01
Rejea za mada hii
Prostate Cancer Foundation. Prostatitis. https://www.pcf.org/about-prostate-cancer/what-is-prostate-cancer/prostate-gland/prostatitis/. Imechukua 20/09/2021
National Kidney and Urological Diseases Information Clearinghouse. Prostatitis: Inflammation of the prostate. https://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/urologic-disease/prostate-problems/Pages/facts.aspx/. Imechukua 20/09/2021
JAMES D. HOLT, MD, et al. Common Questions About Chronic Prostatitis. https://www.aafp.org/afp/2016/0215/p290.html. Imechukua 20/09/2021
Vaidyanathan, et al. “Chronic prostatitis: Current concepts.” Indian journal of urology : IJU : journal of the Urological Society of India vol. 24,1 (2008): 22-7. doi:10.4103/0970-1591.38598
Nickel, J Curtis. “Prostatitis.” Canadian Urological Association journal = Journal de l'Association des urologues du Canada vol. 5,5 (2011): 306-15. doi:10.5489/cuaj.11211