Imeandikwa na ULY CLINIC
20 Septemba 2021 16:37:58
Urethraitiz
Urethritiz hutokana na michomo kwenye mrija wa urethra kama matokeo ya shambulio la kinga ya mwili kwenye vimelea wa maradhi walio kwenye mrija huo haswa wale wanaosababisha magonjwa ya zinaa.
Dalili zake ni;
Kutokwa na uchafu mwembamba na msafi kama kamasi au
Kutokwa na uchafu mzito kama usaha
Dalili zignine ni
Kusita kukojoa
Kushindwa kuzuia mkojo
Kukojoa mara kwa mara
Maumivu wakati wa kukojoa
Muwasho kwenye tundu la mkojo
Hisia za kuungua kwenye tundu la mkojo
Kisababishi kikuu cha urethraitiz ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwenye mrija urethra. Bakteria hao ni kama vile;
Chlamydia trachomatis
Neisseria gonorrhoeae
Vimelea weingine wanaoweza kuchangia lakini kwa asilimia chache ni;
Mycoplasma genitalium
Trichomonas vaginalis
Herpes Simplex virus
Treponema pallidum
Neisseria meningitides
Ureaplasma urealyticum
Ureaplasma parvum
Candida species
Visababishi
Kuna visababishi vingine ambavyo havihusiani na maambukizi pia vinaweza kupelekea tatizo la urethraitiz kama vile;
Uharibifu kwenye njia ya mkojo kutokana na kuwekewa mpira au kifaa tiba kwenye njia ya mkojo au sababu zingine
Uchokozi kwenye njia ya mkojo kutokana na
Kuingiziwa mpira wa mkojo na kukaa muda mrefu
Msuguano kwenye njia ya mkojo kutokana na kuvaa nguo za kubana au shinikizo wakati wa kujamiana
Kufanya kazi za kuongeza shinikizo kwenye njia ya mkojo kama vile kuendesha baiskeli
Matumizi ya sabuni, poda na viuaji manii vyenye uchokozi kwenye ngozi na mrija wa mkojo
Kuingia koma hedhi na kutokuwa na kiwango cha estrogen ya kutosha ( kwa wazee)
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022 19:16:21
Rejea za mada hii
NHS. Overview. Non-gonococcal urethritis. https://www.nhs.uk/conditions/non-gonococcal-urethritis/. Imechukuliwa 20/09/2021
JOHN R. BRILL, MD, MPH. Diagnosis and Treatment of Urethritis in Men. https://www.aafp.org/afp/2010/0401/p873.html. Imechukuliwa 20/09/2021
NCBI. Urethritis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537282/. Imechukuliwa 20/09/2021
Young A, Toncar A, Wray AA. Urethritis. 2021 Jul 29. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2021 Jan–. PMID: 30725967.