top of page

Dalili, viashiria na visababishi

Katika kurasa hizi utasoma kuhusu  dalili, viashiria na visababishi vyake. Kwa maelezo zaidi ya dalili ingia kwenye vipengele vya dalili za ugonjwa ndani ya tovuti hii

Edema ya ghafla ya mapafu

Edema ya ghafla ya mapafu

Husababisha kupumua kwa shida, haraka na kwa ugumu kwenye pozi la kulala, miruzi na kikohozi chenye makohozi ya rangi waridi yenye povu. Wagonjwa pia huonyesha moyo kwenda kasi, wasiwasi, ngozi baridi na yenye ubluu.

Nimonia

Nimonia

Nimonia inayosababishwa na bakteria husababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua. Kawaida, maambukizi haya huanza ghafla na homa kali pamoja na baridi kali.

Emfisema

Emfisema

Ni aina ya COPD inayosababisha kupumua kwa shida, midomo mruzi, kupumua haraka, na kifua cha pipa. Wagonjwa pia huonyesha ishara ya kupungua uzito, vidole rungu na bluu ya pembezoni.

bottom of page