top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

5 Oktoba 2024, 07:09:38

Image-empty-state.png

Dalili za hatari wakati wa ujauzito

Wakati wa ujauzito, afya ya mtoto tumboni ni ya kwanza kuzingatiwa  ndo maana matatizo ya ujauzito yanaweza kuwa ya kuogopesha kwa sababu usipokuwa makini unaweza kupoteza ujauzito ama kujifungua mtoto mwenye matatizo.


Kama una magonjwa sugu kama kisukari, kifafa au huzuniko(depression) unatakiwa kuelewa jinsi gani magonjwa haya yanaweza kudhuru afya yako na mtoto au unatarajia madhara gani kutokana na magonjwa hayo na kujua kinagaubaga kuhusu matibabu yake na jinsi yanavyomwathiri mtoto. Ukijua haya unaweza kuzuia madhara kwa mtoto


Hata kama matatizo yanaweza kuwa makubwa sana katika kichwa chako, mtaalamu wa afya anaweza kufanya liwezekanalo kuhakikisha kwamba unakuwa na ujauzito wenye afya njema na unatakiwa ugndue umuhimu wao na ufanye maamuzi sahihi ya kuonana nao ili upate msaada unapohitajika


Baadhi ya dalili hatari wakati wa ujauzito zimeorozeshwa hapa chini, upatapo dalili hizi onana na mtaalamu wa afya haraka


  • Kutokwa na maji ya uzazi-kupasuka kwa chupa ya uzazi mapema zaidi katika ujauzito

    • ​Chupa ya uzazi kupasuka huwa si kitu rahisi na tatizo hili linapotokea linaweza kumaanisha maambukizi katika kuta za chupa ya uzazi au mgandamizo kwenye tumbo uliosababishwa na kupigwa, kuangukia tumbo au kitu chochote kinachoweza kuleta mgandamizo wa nguvu tumboni

    • Chupa ya uzazi ikipasuka inakuweka hatarini kupata maambukizi kwenye kizazi na mtoto hivyo huweza kusababisha ujauzito kutoka


  • Kutokwa na damu kipindi cha ujauzito

    • ​Kutokwa na damu kipindi cha ujauzito huweza kumaanisha jambo la hatari au lisilo la hatari linaendelea mwilini. Kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ambapo kondo la nyuma huwa linatengenezwa kwa kuvamia ukuta wa uzazi huweza kusababisha mwanamke kuona damu lakini huwa sio nyingi sana wala hakuna maumivu ya tumbo. Endapo damu inatoka sana onana na mtaalamu wa afya upate kufanyiwa uchunguzi

    • Mambo mengine yanayoweza kusababisha damu katika ujauzito ni Saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi,

​

  • Maumivu ya kichwa kutapika kupita kiasi au shinikizo la damu la juu, maumivu ya tumbo na kutoona vizuri(kuona vitu vimefifia)

    • ​Dalili hizo zinaweza kumaanisha mama amepata shinikizo la damu linaloelekea kuwa kifafa cha mimba au kitaalamu preeclampsiaau,shinikizo la damu la damu sugu na kifafa cha mimba/eclampsia.

    • Maumivu ya tumbo ya kubana na upande mmoja wa nyonga na maumivu kwenye bega la kizunguzungu kichefuchefu na kutapika miezi  mitatu ya kwanza ya ujauzito, mara nyingi hutokea kama mimba imetungwa nnje ya mfuko wa kizazi. Mama na awahi hospitali kwa uchunguzi zaidi ili kuondokana na matatizo ya kuvilia damu kwenye tumbo mara baada ya ujauzito huo kupasuka na hivyo kupoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi


  • Kutokwa na uchafu unaonuka ukeni

    • ​Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuleta dalili kama hii, maambukizi pia katika uke au mfuko wa kizazi huweza kusababisha pia. Mama ni vema kwenda kituo cha afya kwenda kupima afya yake


  • Maumivu makali ya tumbo ya kubana mapema zaidi katika miezi mitatu ya pili ya ujauzito

    • ​Maumivu ya tumbo kabla ya wiki 37 za ujauzito humaanisha kuanza kwa uchungu kabla ya muda kufika (preterm labor) tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama vile magonjwa sugu ya mama (kisukari kisicho dhibitiwa), maambukizi ya uke au kizazi au wakati mwingine kama mama ana mapacha tumboni. Ni vema kujua kuhusu afya yako kwa kumtafuta mtaalamu wa afya akufanyie vipimo na matibabu kama yatahitajika

​

  • Mtoto kupunguza kucheza au kutocheza tumboni kuanzia kipindi cha miezi 

    • ​​Kuanzia wiki ya ishirini ya ujauzito mara nyingi mtoto huanza kucheza tumboni kwa mama, mtoto kucheza huonyesha mtoto yupo hai na anakua vyema. Mama anatakiwa kujua namna mtoto wake anavyocheza ili akigundua mtoto amepunguza kucheza basi aonane na mtaalamu wa afya. Mtoto kutocheza au kupunguza kucheza huweza kumaanisha mtoto amefia tumboni ama mimba ilishatoka

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

5 Oktoba 2024, 07:09:38

Rejea za dawa

  1. NCBI-Counselling for Maternal and Newborn Health Care: A Handbook for Building Skills. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304178/. Imechukuliwa 05.10.2024

  2. CDC. https://www.cdc.gov/hearher/maternal-warning-signs/index.html.  Imechukuliwa 05.10.2024

  3. UNICEF danger sign in pregnancy. https://www.unicef.org/timorleste/media/2386/file/Danger%20signs%20for%20women%20-%20English%20.pdf. Imechukuliwa 05.10.2024

bottom of page