top of page
Surua-ulyclinic

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

Dalili za Surua

Surua kwa jina la kitiba(measles) husababishwa na maambukizi ya kirusi aitwaye measles

Dalili na viashiria vya surau huanza kuonekana siku ya 10 hadi 14 toka maambukizi kutokea, na dalili huhusisha

  • Homa- hupanda hadi kufikia nyuzi joto za selicias 40 na 41

  • Kikohozi kikavu

  • Kuchuruzika mafua

  • Kuhisi Koo kavu

  • Macho kuwa mekundu na kuuma(konjaktivaitis)

  • Doti za Koplik’s

  • Vipele kwenye Ngozi ambavyo huanza kutokea usoni kwanza na kufuata kwenye mwili mikono mabega, mapajani na miguuni. Na hupotea kwa kufuata mtiririko huo

Dalili zisizo maalumu ni kama vile

 

Homa kiasi inayoambatana na kikohozi, kutokwa na mafua, macho kuwa mekundu, na kinywa kikavu ambapo dalili zinaweza kukaa kwa muda wa siku tat una kuondoka.

Maambukizi kwa watu wengine yanaweza kutokea muda wa siku tano, ikianza na siku moja kabla ya vipelekutokea.

Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii

Imeboreshwa mara ya mwisho 11.03.2020

Rejea

soma zaidi kuhusu dalili za surua na surua kwa kubonyeza hapa

Imeboreshwa 24.03.2020

bottom of page