Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali
ULY Clinic inakushauri kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Dalili za gono kwa mwanamke
Ni wanawake wachache (≈ 20–50 %) wanaopata gono huonyesha dalili, ambazo hujumuisha ute/usahu ukeni wenye harufu au rangi isiyo kawaida na maumivu wakati wa tendo la ndoa. Gono hutibiwa kwa antibiotiki mseto; daima pata uchunguzi na ushauri wa daktari kabla ya kuanza tiba yoyote.

Maumivu ya chembe ya moyo
Maumivu ya chembe ya moyo yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya tumbo au via vingine ndani ya kifua, kama vidonda vya tumbo, au kucheua tindikali. Matibabu yanategemea chanzo cha maumivu na yanaweza kujumuisha dawa, mabadiliko ya mtindo wa maisha, na, wakati mwingine, upasuaji.