top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

21 Machi 2020, 09:01:49

Dalili za Gono(kisonono)
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za Gono(kisonono)

Kisonono husababishwa na Bacteria aitwaye Neisseria gonorrhoeae. Pia ugonjwa huu huweza kuambukiza kutoka kwa mama kwenda kwa mototo mchanga pale anajifungua.


Bacteria huyu hushambulia sana kwenye njia ya mkojo na via vya uzazi kwa mwanaume na mwanamke na ukuta wa macho uitwao konjaktiva. Gono huweza kusababisha matatizo ya uzazi (utasa) kwa mgonjwa endapo asipopata matibabu mapema.


Dalili za gono


Dalili za Gono huanza kuonekana kati ya siku 2 mpka 10 baada ya maambukizi, pia kwa wanaume hua inahusiana na kwenye mrija unaotoa mkojo(njia ya mkojo)


Dalili za gono kwa wanaume

  • Dalili za mwanzo ni muwasho katika tundu la njia ya mkojo

  • Maumivu ya kuungua njia ya mkojo wakati wa kukojoa

  • Kutokwa na usaha kwenye njia ya mkojo

  • Kushindwa kabisa kupitisha mkojo

  • Kupitisha mkojo kwa shida ambapo itakua inazid kadri siku zinavyoenda

  • Kuonekana kwa damu kwenye mkojo


Dalili za gono kwa wanawake

Zaidi ya asilimia 50 mpaka 80 ya wanawake walioambukizwa ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili zozote zile, hivyo ni vigumu kutambulika mapema.


Dalili zifuatazo huonekana kama matokeo ya Gono

  • Kutoka ute, Uasaha au maji machafu yenye harufu kali ukeni

  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa


Madhara ya gono kwa wanaume

Kuharibika kwa njia ya kupitisha mkojo na shahawa hivyo uwezekano wa kushindwa kupata mtoto.


Madhara ya gono kwa Wanawake

  • Maambukizi kwenye via vya Uzazi

  • Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

  • Maambukizi kwenye mirirja ya Mayai

  • Kuharibika kwa Mimba

  • Kushindwa kupata watoto


Namna ya kujikinga na ugonjwa wa gono


Jikinge Gono kwa kufanya mambo yafuatavyo;


  • Kutokufanya ngono zembe

  • Epuka mahusiano ya mpenzi zaidi ya mmoja

  • Fahamu na fanya Matumizi sahihi ya kondomu

  • Unapopata dalili za Gono wahi ukapimwe ili ugonjwa ugunduliwe na kutibiwa mapema bila kuleta

  • madhara.

  • Endapo umetambulika kuwa una gono, hakikisha wapenzi wako wote wanatibiwa kwa kuwa wasipotibiwa watakuambukiza tena

  • Penda kujisomea kuhusu magonjwa ya zinaa ili kupata elimu zaidi na zaidi

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023, 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Cook. G., & Zumla, A. (2003). Manson’s Tropical Diseases, 21st ed.). London: Saunders.
2.Haslett C., Chilvers R.E e.t al (Ed), (2000). Davison’s Principle and Practice of Medicine, 20th edition.
Churchill and Livingstone. UK: Edinburg.

3.Kingondu, T. et al, (2007). (2008). Communicable Disease. Nairobi, Kenya. AMREF

4.NACP and RCH Section (2007). National Guidelines for Management of Sexually Transmitted and
Reproductive Tract Infections (1st ed.). Dar es Salaam, Tanzania: Ministry of Health and Social Welfare,
National AIDS Control Programme Reproductive and Child Health.

5.Gonorrhea and chlamydia: Screening. (2014, September
uspreventiveservicestaskforce.org/Page/Document/RecommendationStatementFinal/chlamydia-and-
gonorrhea-screening

6.Gonorrhea - CDC fact sheet (detailed version). (2015, November 17)
cdc.gov/std/gonorrhea/stdfact-gonorrhea-detailed.htm

7.Kumar, P. (2012, January-June). Gonorrhoea presenting as red eye: Rare case. Indian Journal of Sexually
Transmitted Diseases and AIDS, 33(1), 47-48 ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3326851/

bottom of page