Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
27 Machi 2020 21:02:05
Dalili za Maleria kali
Maleria ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya kimelea cha protozoa aitwaye plasmodium falciparum, mtu hupata maambukizi ya kimelea huyu kwa kung'atwa na mbu jike aitwaye anoferesi, njia zingine ni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni au kwa njia ya kuongezewa damu na kutumia sindano na mtu mwenye malaria haswa kwa watu wanaotumia madawa ya kulevya. Mbu huyu hupatikana hasa nyakati za usiku wa manane.
Maleria sugu hufahamika kama malaria ya muda mrefu kwa watu wenye kinga ya mwili ya kati, bila kuwa na dalili ya homa au dalili zingine. Maleria hii isipotibiwa huweza kuibiku na kuleta maleria yenye mwitikio wa slenomegali ambayo ni malaria hatari sana.
Ugonjwa huu huwapata watu wa jinsia zote, waume kwa wake. Lakini pia ugonjwa huu huweza kuleta vifo kwa watoto na wamama wajawazito.
Dalili za malaria Kali
Degedege
Kuchanganyikiwa
Kukojoa mkojo wenye rangi ya koka kola
Kuishiwa damu mwilini
Manjano ya macho
Kupata shida ya kupumua
Kushuka kwa glukosi mwilini
Figo kuferi ghafla
Homa kali
Kuvimba kwa tumbo kutokana na kuvimba kwa bandama
Hatua za kuchukua ili kuepukana na malaria
Kulala kwenye chandarua chenye dawa ya kuua mbu
Kufukia madimbwi na mabwawa yote karibu na makazi
Kufyeka vichaka kuzunguka nyumba ili kuondoa mazalia ya mbu
Kufuata maelezo ya wataalamu wa afya kuhusiana na malaria
Kutumia dawa za kupaka za kufukuza mbu kama Dawa zenye DEET
Kuvaa nguo zinazofunika mwili wakati wa usiku kama nguo zenye mikono mirefu, suruali pamoja na soksi
Matumizi ya dawa za kujikinga na malaria endapo unasafiri kwenda nchi zenye malaria
Kuonana na daktari mapema mara unapopata dalili na viashiria vya malaria
Kupata chanjo ya malaria ya RTS, S/AS01 endapo itakubalika kutumika na WHO(chanjo bado ipo
mkwenye majaribio)
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Zeno Bisoffi etal. Malaria journal. Chronic malaria and hyper-reactive malarial splenomegaly: a retrospective study on the largest series observed in a non-endemic country https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4839070/. Imechukuliwa 27.03.2020
2.WHO. Overview malariaof treatment. https://www.who.int/malaria/areas/treatment/overview/en/ Imechukuliwa 27.03.2020
3.Jameson JL, et al., eds. Malaria. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 27.03.2020
4.Tintinalli JE, et al., eds. Malaria. In: Tintinalli's Emergency Medicine: A Comprehensive Study Guide. 8th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2016. http://www.accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 27.03.2020
5.Malaria. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/infectious-diseases/extraintestinal-protozoa/malaria. Imechukuliwa 27.03.2020
6.Malaria. Centers for Disease Control and Prevention. http://wwwnc.cdc.gov/travel/diseases/malaria. Imechukuliwa 27.03.2020
7.Breman JG. Clinical manifestations of malaria in nonpregnant adults and children. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 27.03.2020
8.Daily J. Treatment of uncomplicated falciparum malaria in nonpregnant adults and children. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 27.03.2020
9.Key points: World malaria report 2017. World Health Organization. https://www.who.int/malaria/media/world-malaria-report-2017/en/. Imechukuliwa 27.03.2020