Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
22 Machi 2020 22:28:26
Dalili za Saratani ya mapafu
Saratani ya mapafu Ni ugonjwa unaohusishwa na ukuaji wa seli bila mpangilio katika tishu za mapafu. Seli hizi za saratani zinaweza kuenea kwa njia inayoitwa metastaisi kwenda kwenye tishu zilizokaribu na seli hizi za saratani au mbali Zaidi na seli hizo
Mapafu ni ogani ya mwilini yenye kazi kubwa ya kuingiza hewa safi ya okseji mwilini na kutoa hewa ya chafu ya kaboni dayoksaidi nje ya mwili.katika mfumo wa upuaji mapafu ni ogani kubwa Zaidi kulinganisha na ogani zingine mwilini. Mapafu yanapatikana ndani ya kifua chini ya uvungu wa mbavu na huwa yamekaa katika pande mbili kushoto na kulia huku moyo ukiwa umekaa katikati ya mapafu hayo.
Pafu la kulia lina sehemu 3 na Pafu la kushoto lina sehemu 2. Kila sehemu inajitegemea bila kuhusiana na nyinginezo. Hivyo upasuaji unaweza kufanyika kutoa sehemu moja ya pafu bila kuathiri kwa kiasi kikubwa upumuaji wa mtu.
Visababishi
Visababishi vya Saratani ya mapafu
Uvutaji wa sigara—hiki ni kisababishi kikuu cha saratani ya mapafu katika asilimia 90%
Uchafuzi wa hewa uliokithiri, mfano unaosababishwa na moshi kutoka viwandani
Mionzi
Gesi yenye sumu mfano gesi ya methyl ether
Madini ya Uranium
Dalili za Saratani ya mapafu
Kukohoa mara kwa mara
Kukohoa damu
Maumivu ya kifua wakati wa kupumua ama kukohoa
Kuishiwa na pumzi ama matatizo ya upumuaji
Kupoteza uzito bila sababu ya msingi
Homa za mara kwa mara
Maambukizi ya mara kwa mara kwenye mapafu mfano nimonia
Kukosa hamu ya kula
Sauti kutoka na mikraruzo
Kelele kwenye kifua wakati wa kuvuta na kutoa hewa kutokana na njia za mapafu kuzibwa na saratani
Dalili na Ishara ya Saratani ya mapafu iliyosambaa
Maumivu ya mifupa kwenye mbavu, mgongo na nyonga- Inaashiria saratani imesambaa kwenye uti wa
mgongo na nyonga
Kuvimba kwa Uso na Shingo- saratani imesambaa kichwani
Mabadiliko katika mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kupoteza
fahamu, ganzi katika mikono na miguu- saratani kusambaa kwenye mfumo wa fahamu wa kati na pembeni
Rangi ya manjano katika macho na ngozi - saratani imesambaa katika Ini
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Lung cancer at https://www.google.com/url?q=https://www.cancer.org/cancer/lung-cancer/detection-
diagnosis-staging/signs
symptoms.html&sa=U&ved=2ahUKEwiS06Wp3qvoAhXohXIEHVlUBogQFjAOegQIAxAB&usg=AOvVaw13iPkN5RKkkhxulqj96nm. Imechukuliwa 21.3.2020
2. Lung cancer basic information at https://www.google.com/url?q=https://www.cdc.gov/cancer/lung/basic_info/what-is-lung-cancer.htm&sa=U&ved=2ahUKEwiS06Wp3qvoAhXohXIEHVlUBogQFjAWegQICBAB&usg=AOvVaw3U4PxoVyzgO4SWGbDIR6RA. Imechukuliwa 21.3.2020
3. Lung cancer symptoms at https://www.google.com/url?q=https://www.nhs.uk/conditions/lung-cancer/symptoms/&sa=U&ved=2ahUKEwjPuYzq4avoAhUCgXIEHVxZB0AQFjANegQIARAB&usg=AOvVaw1BN5-3cUHABN-_gg7NWiRf. Imechukuliwa 21.3.2020
4. Lung cancer understanding at https://www.google.com/url?q=https://www.webmd.com/lung-cancer/understanding-lung-cancer-symptoms&sa=U&ved=2ahUKEwjPuYzq4avoAhUCgXIEHVxZB0AQFjAPegQICBAB&usg=AOvVaw0YOet9aShImi4M2vxPQFfv. Imechukuliwa 21.3.2020
5. Lung cancer symptoms at https://www.google.com/url?q=https://www.cancercenter.com/cancer-types/lung-cancer/symptoms&sa=U&ved=2ahUKEwjPuYzq4avoAhUCgXIEHVxZB0AQFjALegQIChAB&usg=AOvVaw1tvgfmPW_SbZZWTeoGj3vV. Imechukuliwa 21.3.2020