Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, M.D
20 Machi 2020, 17:17:18
Dalili za Taifodi
Mtu anapata maambukizi ya homa ya matumbo (typhoid fever) kwa kula chakula au kunywa maji yaliyo na viini wa vimelea vya bakteria. Vimelea wa taifodi hupatikana kwenye kinyesi na mkojo wa mtu.
Kula vyakula ambavyo vimeandaliwa pasipo usafi, au chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi, kutumia mayai mabichi au ambayo hayajaiva vema, na chakula ambacho hakijapikwa na kuiva hukuweka kwenye kihatarishi cha kupata maambukizi haya. Tafiti zinaonyesha kwamba bakteria huyu huweza kujificha kwenye kwenye Ini la binadamu na mayai ya kuku, hivyo maambukizi yanaweza kutokea kwa kula mayai au maini ambayo hayajapikwa vema.
Mgonjwa wa homa ya Matumbo anaweza asiwe na dalili lakini akaweza kuwaambukiza wengine.
Mgonjwa wa Taifodi huchukua siku 10 mpaka 14 kuonyesha dalili za taifodi, hata hivyo muda wa kuonyesha dalili toka maambukizi yametokea hutegemea dose (wingi) ya wadudu wa taifodi alionao. Dalili za taifodi huanza taratibu mfano Homa kutoka jasho muda na muda, maumivu ya tumbo, kuharisha kidogo kidogo japo muda na muda mwingine huambatana na damu kidogo.
Dalili za Taifodi (homa ya matumbo)
Dalili za mwanzo kabisa ni kama maumivu ya kichwa, kukosa hamu kula, kichefuchefu, maumivu ya mwili na uchovu.
Pamoja na hivyo Mgonjwa asipotibiwa mapema, dalili zingine huweza kutokea kutokana na taifodi kuwa sugu.
Dalili za taifodi katika wiki ya kwanza
Maumivu ya kichwaa
Uchovu wa Mwili
Homa za kupanda na kushuka
Kukosa choo
Kikohozi kwa mbali
Dalili za taifodi katika wiki ya pili
Homa kuzidi kupanda na kupelekea moyo kwenda taratibu
Kuharisha
Tumbo kuvimba na maumivu kwenye Bandama
Dalili za taifodi katika wiki ya tatu
Kuzidi Kuharisha kinyesi cha njano
Kushuka kwa Homa
Kuchanganiyikiwa (Kama mtu mwenye kichaa)
Kuvimba kwa tumbo au
Kutoboka kwa utumbo mwembamba
Katika hatua hii ya tatu kifo huweza kutokea kutokana na madhara yaliyoorodheshwa.
Madhara ya taifodi
Yafuatayo ni madhara/matokeo ya kiafya yatokanayo na taifodi(homa ya matumbo) kama isipo tibiwa
Kutoboka kwa utumbo
Kuvuja damu
Homa ya uti wa mgongo
Maambukizi ya kifuko cha nyongo
Muhimu
Taifodi hutibika kama magonjwa mengine hivyo unashauriwa kudumisha usafi wa mazingira, na umakini wakati wa kuandaa vyakula.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:04:19
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Cook, G., & Zumla, A. (2003). Manson’s Tropical Diseases, (21st ed.). London: Saunders.
2. Kingondu, T. et al, (2007). Communicable Diseases. (2008). Nairobi : AMREF
3. Engels, E. A., Falagas, M. E., Lau, J., & Bennish, M. L. (1998). Typhoid fever vaccines: a meta-analysis of studies on efficacy and toxicity. BMJ. 1998;316:110 http://www.bmj.com/content/316/7125/110
4. Scientists get a handle on what made Typhoid Mary's infectious microbes tick.(2013, August 14)
https://med.stanford.edu/news/all-news/2013/08/scientists-get-a-handle-on-what-made-typhoid-marys-infectious-microbes-tick.html
5. Levy, S. B. (2002). Factors impacting on the problem of antibiotic resistance. Journal of Antimicrobial Chemotherapy. Volume 49, Issue 1Pp. 25-30 http://jac.oxfordjournals.org/content/49/1/25.full
6. Sharma, A. K., Sharma, R. K., Sharma, S. K., Sharma, A., & Soni, D. (2013, November). Typhoid intestinal perforation: 24 perforations in one patient. Annals of Medical and Health Sciences Research. 3(Suppl1): S41–S43 http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3853607/