top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY Clinic

25 Juni 2020, 18:20:59

Dalili za kifafa
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za kifafa

Kifafa huelezewa kuwa ni degedege la kujirudia rudiarudia, degedege hili husababisha mwili kojongesha misuli bila hiaria mithiri ya mtu aliye na pepo au kupigwa na shoti ya umeme.


Kifafa kinaweza kuwapata watu wakubwa, watoto wadogo, jinsia yeyote na katika umri wowote.


Vihatarishi vya kupata kifafa


  • Kukosa usingizi kwa muda mrefu

  • Kuwa na historia ya kifafa kwenye ukoo au familia

  • Msongo wa mawazo

  • Taa za kimurimuri mfano televisheni, Taa za Disko

  • Kutokunywa dawa za kifafa kama ulivyopangiwa na mtaalamu wa afya

  • Matumizi ya dozi kubwa ya dawa kama haloperidol,chlorpromazine

  • Matumizi ya pombe na dawa za kulevya kama vile kokeini

  • Kiwango kidogo cha sukari mwilini


Visababishi vya kifafa


Kwa watoto wachanga/wadogo

  • Sababu za kimaumbile

  • Kasoro/matatizo wakati wa kuzaliwa mfano kukosa hewa oksijeni wakati wa kuzaliwa

  • Homa ya Uti wa mgongo

  • Majeraha ya wakati wa kuzaliwa

  • Matatizo ya mishipa ya fahamu

  • Saratani au uvimbe ndani ya fuvu la kichwa

  • Homa kali za mara kwa mara


Kwa vijana na umri wa kati

  • Jeraha kichwani

  • Saratani ya ubongo

  • Magonjwa ya mfumo wa fahamu


Kwa wazee

  • Kiharusi

  • Matatizo katia mfumo wa neva

  • Saratani ya ubongo

  • Majeraha kichwani


Dalili za kifafa


  • Kuchanganyikiwa kwa muda

  • Mijongeo ya misuli ya mwili isiyo ya hiari

  • Kupoteza fahamu

  • Kutoelewa mazingira

  • Dalili za ukichaa kama hofu, shauku kuu

  • Dalili za déjà vu


Dalili zinazoambatana na kifafa

Dalili zingine zinazoambatana ni


  • Mkojo au kinyesi kutoka chenyewe

  • Kutokwana povu mdomoni

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021, 04:52:13

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.MOHSW (2005). Tanzania National Formulary. Dar es Salaam, Tanzania: Ministry of Health and Social Welfare.

2.Braunwald, E. & Fauci, A.S. (2001). Harrison’s Principles of Internal Medicine. McGraw Hill

3.Boom, N. A., Colledge, N.R., Walker, B.R. et al. (2006). Davidson’s Principles and Practices of Medicine. Churchill, Livingstone.

4.Fischer, J.H. (1994). The Epilepsy Counseling Guide. Fair Lawn: New Jersey

bottom of page