Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
27 Machi 2020 17:48:02
Dalili za magonjwa ya figo
Magonjwa ya figo ni mjumuiko wa magonjwa yote yanayoathiri utendaji kazi wa figo. Baadhi ya magonjwa ya figo huweza kwenda mpaka miezi mitatu bila kuleta dalili za kushitukiza kuwa mtu ana tatizo la figo ila mtu huwa na upungufu wa ufanyaji kazi wa figo.
Magonjwa ya figo huweza kuwapata watu wote wake kwa waume na kwa rika zote.
Visababishi
Magonjwa ya figo huweza kusababisha na vitu vifuavyo;
Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
Maambukizi kwenye glumerula
Mawe kwenye figo
Ugonjwa wa UTI yenye kujirudia rudia
Kuziba kwa nefroni
Kuziba kwa mirija ya mikojo kama kunakosababishwa na tezi dume au mawe kwenye njia za mkojo
Mambukizi kwenye mishipa ya gromerula pamoja na nefroni
Sumu, chakula au dawa
Ajali /Kuumia eneo la figo
Tatizo la kurisi la ugonjwa wa Figo wa polisistiki
Dalili za magonjwa ya figo
Uso Kuvimba wakati unaamka asubuh au wakati wote au uvimbe kuzunguka macho
Kuvimba kwa miguu
Mwili kuvimba mzima
Mkojo kutoa povungozi kukauka na kuwasha
Uchovu wa mwili na kuishiwa nguvu
Kushindwa kuwa makini
Kushindwa kupata usingizi
Kutokwa damu kwenye mkojo
Kukojoa mara kwa mara
Maumivu ya magoti
Kuonekana kwa protini kwneye mkojo wa mgonjwa
Maumivu ya mwili
Kuvimba kiwiko chamkono na magoti
Kichefuchefu
Kutapika
Uchovu kupita kiasi
Maumivu ya kifua kama maji yametuwama kwenye moyo
Kuishiwa pumzi kama maji yametuwama kwenye mapafu
Shinikizo la juu la damu lililogumu kutibika
Vihatarishi vya kupata magonjwa ya figo
Kisukari
Shinikizo la juu la damu
Uvutaji wa sigara
Obeziti
Kuwa muafrika
Historia ya ugonjwa wkenye familia
Figo yenye umbo lisilo la kawaida
Umri mkubwa
Namna ya kujikinga na magonjwa ya figo
Fuata maelekezo ya matumizi ya dawa
Unaponunua dawa dukani hakikisha umeandikiwa na daktari na unafuata maelekezo ya namna ya kutumia, dawa kama aspirini, ibrupofen parasetamol(panado) na dawa zenye mchanganyiko wa parasetamo huweza kuharibu figo na kuleta magonjwa ya figo. Kutumia dawa za Maumivu mara kwa mara kunakuweka hatarini kupata magonjwa na yanatakiwa kutotumika kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa figo.
Uzito
Hkikisha unakula vizuri chakula kinachoshauriwa kiafya na kuishi Maisha yanayoshauriwa kiafya
Fanya mazoezi siku 3 hadi 4 za wiki na kazi za kutoa jasho ili mwili uwe imara. Kama una uzito mkubwa ongea na daktari wako kwa ushauri wa namna gani ya kupunguza uzito na uzito gani unakufaa wewe.
Punguza kiasi cha wanga unaotumia ili kuepuka unene.
Usivute sigara na tumbaku
Sigara hudhuru mishipa ya damu ya figo. Kama unavuta sigara ongea na daktari wako namna gani ya utaweza kuacha kuvuta sigara.
Tibu magonjwa yako kwa kupata ushauri kutoka kwa Daktari
Usijitibu mwenyewe bila kupata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wako. Endapo ugonjwa ulionao unaongeza hatari ya kupata magonjwa ya figo basi ongea na daktari wako namna gani ya kuzuia kupata ugonjwa huu.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Braunwald, E. & Fauci, A.S. (2001). Harrison’s Principles of Internal Medicine. McGraw Hill.
2.Cumming A.D. (2003). Davidson’s Principles and Practice of Medicine. Edinburgh, Oxford: Elsevier Saunders.
3.Kumar, P. & Clark, M. (2007). Clinical Medicine (6th ed.). Edingurgh, Oxford: Elsevier Saunders.
4.National Kidney Foundation. 10. Signs you may have kidney disease. https://www.kidney.org/news/ekidney/august14/10_Signs_You_May_Have_Kidney_Disease Imechukuliwa 27.03.2020
5.Rosenberg M. Overview of the management of chronic kidney disease in adults. http://www.uptodate.com/home. 27.03.2020
6.Coping effectively: A guide for patients and their families. The National Kidney Foundation. https://www.kidney.org/atoz/content/coping_effectively_guide. 27.03.2020
7.Chronic kidney disease: What does it mean for me? National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-communication-programs/nkdep/a-z/kidney-disease-mean-for-me/Pages/default.aspx. 27.03.2020
8.Chronic kidney disease (CKD) and diet: Assessment, management and treatment. National Kidney Disease Education Program. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-communication-programs/nkdep/a-z/Documents/ckd-diet-assess-manage-treat-508.pdf. 27.03.2020
9.Kidney failure: Choosing a treatment that's right for you. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/kidney-disease/kidney-failure-choosing-a-treatment-thats-right-for-you/Pages/facts.aspx. 27.03.2020