Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
27 Machi 2020 19:34:35
Dalili za mimba kuharibika
Miskerieji ni kutoka au kuharibika kwa mimba kabla ya wiki 20 za ujauzito, mimba hii hutoka yenyewe bila kuwa na uchokozi wowote.
Kwa Tanzania mimba ikitoka kabla ya kufikisha wiki 28 za ujauzito huitwa miskerieji. Inakadiliwa kuwa asilimia 10 hadi 20 ya wajawazito hupata miskerieji, namba hii ni ndogo ukilinganisha na hali halisi kwa sababu mimba nyingi hutoka wakati mwingine mapema Zaidi na kudhaniwa ni damu ya hedhi ya kawada au hedhi kuchelewa.
Endapo mimba itatoka baada ya kipindi cha wiki 20 au 28 kama ilivyo Tanzania, tatizo hilo hufahamika kuwa Mtoto kufia tumboni.
Kutoka kwa mimba kumegawanyika katika aina nyingi ambazo zimezungumziwa sehemu nyingine kwenye tovuti hii.
Kumbuka katika mada hii kutoka kwa mimba kunamamanisha pia mimba kuharibika yenyewe
Visababishi
Vipo visababishi aina kadhaa vinavyoweza kupelekea mimba kutoka
Matatizo kwa mtoto
Matatizo ya kufanyika kwa mtoto kama vile madhaifu ya kromosomu ya mtoto
Matatizo kwa mama
Kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kaswende, UKIMWI, maleria, na Rubela
Kuwa na ugonjwa wa kisukari ulioshindikana kudhibitiwa
Matumiziya dawa aina mbalimbali zisizoruhusiwa kutumika wakati wa ujauzito kamaa misopostol n.k
Matatizo ya usawa wa homoni mwilini
Magonjwa ya tezi ya thairoidi
Ajali au jeraha kwenye tumbo mfano kupigwa tumboni n.k
Matatizo ya mfuko wa kizazi
Kuwepo kwa makovu au kuota kwa nyama nyama kwenye mji wa mimba mfano faibroidi
Kutokujiweza kwa Shingo ya kizazi
Matatizo ya maumbile ya mji wa mimba kama kizazi cha bikonyueti
Sababu gani hazisababishi mimba kutoka?
Mazoezi wakati wa ujauzito kama vile kukimbia kulima na kuendesha baiskeli
Kujamiana
Kufanya kazi za kawaida, isipokuwa kufanya kazi kwenye sehemu zenye mionzi au kemikali.
Dalili za mimba inayotoka
Maumivu makali ya tumbo la chini na maumivu ya mgongo, ya kubana yanayoongezeka jinsi muda unavyokwenda
Matone ya damu nyekundu au iliyoganda kutoka ukeni
Kutokwa na majimaji na tishu za mtoto ukeni
Tumbo kutokuongeeka ukubwa licha ya miezi kwenda mbele
Kupotea kwa mapigo ya moyo ya mtoto
Mtoto kuacha kucheza tumboni
Maumivu makali ya kichwa
Vihatarishi vya mimba kutoka
Umri
Kupata mimba kwenye umri Zaidi ya miaka 35 inaleta hatari kubwa ya kutoka kulinganisha na mimba ambazo zimetokea chini ya umri huo. Kupata mimba kwenye umri Zaidi ya miaka 35
kunaongeza hatari mara 20 zaidi ya miskerieji, umri wa miaka 40 huongeza mara 40 zaidi na umri wa miaka 45 huongeza hatari mara 80 zaidi tatizo la miskerieji.
Kuwa na historia iliyopita ya miskerieji
Kuwa na historia ya mimba kutoka mara moja au mbili
kunakuweka hatarini Zaidi kutokwa na mimba inayofuata. Unahitajika kufanyiwa uchunguzi ili kujua tatizo linalosababisha mimba kutoka kabla ya kupata mimba ingine.
Magonjwa sugu
Magonjwa sugu kama kisukari kisichodhibitiwahuchangia mimba kuharibika.
Matatizo ya mfuko wa kizazi
Kama kutojiweza kwa shingo ya kizazi na kizazi cha baikonyueti.
Uzito mkubwa
Kuwa na uzito mkubwa au uzito mdogo kupita kaisi (soma zaidi kuhusu BMI kujua kuhusu uzito mkubwa na uzito mdogo kupita kaisi kwenye sehemu nyingine kwenye tovuti hii)
Sumu
Kutoka kwenye uvutaji wa sigara na tumbaku pamoja matumizi ya dawa za kulevya.
Vipimo
Baadhi ya vipimo kama vile kipimo cha amniosentesisi kinachochukua sampuli kutoka ndani ya tumbo la ujauzito, kwa nadra huweza kusababisha mimba kutoka.
Madhara
Madhara ya kutoka kwa mimba endapo hayatatibiwa yamegawanyika katika sehemu mbili, madhara ya muda mfupi na madhara ya muda mrefu.
Madhara ya awali
Kutokwa damu ukeni
Maambukizi ya Bakteria kwenye kizazi
Kuishiwa na Damu
Madhara ya baadae
Maambukizi kwenye via vya uzazi
Utasa
Maaumivu makali ya kizazi na ya muda mrefu
Kuathirika kisaikolojia
Namna ya kujikinga dhidi ya mimba kutoka
Inawezekana kuwa vigumu wakati mwingine kujikinga na mimba kuharibika endapo sababu hazifahamiki.
Kufanya mambo yafuatayo yanaweza kukuondoa kwenye hatari ya mimba kuharibika na kutoka
Hudhuria kliniki kabla ya kupata ujauzito kupata ushauri wa daktari na vipimo mbalimbali.
Jikinge na vihatarishi vinavyosababisha mimba kutoka
Hudhuria kliniki baad ya kupata ujauzito kama ulivyopangiwa
Kunywa dawa za nyongeza za mativitamini
Punguza kiwango cha kahawa unachokunywa
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Oats, J., Abraham, S. (2005) Llewellyn-Jones Fundamentals of Obstetrics and Gynaecology. (8th Ed.). Edinburgh: Mosby. MOHSW. (2005).
2.Advanced LSS Trainee Manual. Dar es Salaam, Tanzania: Ministry of Catalano PM. Obesity in pregnancy. In: Gabbe SG, Niebyl JR, Simpson JL, et al, eds. Obstetrics: Normal and Problem in Pregnancies. 7th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2017: chap 41.
3.Hobel CJ, Williams J. Antepartum care. In: Hacker NF, Gambone JC, Hobel CJ, eds. Hacker & Moore's Essentials of Obstetrics and Gynecology. 6th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2016:chap 7.
4.Keyhan S, Muasher L, Muasher S. Spontaneous abortion and recurrent pregnancy loss; etiology, diagnosis, treatment . In: Lobo RA, Gershenson DM, Lentz GM, Valea FA, eds. Comprehensive Gynecology. 7th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2017:chap 16.
5.Moore KL, Persaud TVN, Torchia MG. Discussion of clinically oriented problems. In: Moore KL, Persaud TVN, Torchia MG, eds. Developing Human, The. 10th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2016:503-512.
6.Nussbaum RL, McInnes RR, Willard HF. Principles of clinical cytogenetics and genome analysis. In: Nussabaum RL, McInnes RR, Willard HF, eds. Thompson & Thompson Genetics in Medicine. 8th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2016:chap 5.
7.Tulandi T, et al. Spontaneous abortion: Management. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 27.03.2020.
8.What is recurrent pregnancy loss (RPL)? American Society for Reproductive Medicine. https://www.asrm.org/uploadedFiles/ASRM_Content/Resources/Patient_Resources/Fact_Sheets_and_Info_Booklets/recurrent_preg_loss.pdf. Imechukuliwa 27.03.2020.
9.Huffman CS, et al. Couples and miscarriage: The influence of gender and reproductive factors on the impact of miscarriage. Women's Health Issues, 2015;25:570.
10.Para A, et al. Exercise and pregnancy loss. American Family Physician. 2015;91:437. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 27.03.2020
11.Moscrop A. Can sex during pregnancy cause a miscarriage? A concise history of not knowing. British Journal of General Practice. 2012;62:e308. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3310038/. Imechukuliwa 27.03.2020
12.Risk factors for miscarriage from a prevention perspective: A nationwide follow-up study. BJOG: An international journal of obstetrics and gynaecology. 2014;121:1375. https://www.clinicalkey.com/#!/content/medline/2-s2.0-24548778. Imechukuliwa 27.03.2020
13.Louis GMB, et al. Lifestyle and pregnancy loss in a cohort of women recruited before conception: The LIFE study. Fertility and Sterility. In press. Imechukuliwa 27.03.2020.
14.Early pregnancy loss. American College of Obstetricians and Gynecologists. http://www.acog.org/-/media/For-Patients/faq090.pdf. Imechukuliwa 27.03.2020
15. ACOG Practice Bulletin Number 200: Early pregnancy loss. November 2018. American College of Obstetricians and Gynecologists. Obstetrics and Gynecology. 2018;132:e197.