top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

12 Novemba 2020 11:39:54

Dalili za ugonjwa wa moyo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za ugonjwa wa moyo

Magonjwa ya moyo ni moja ya magonjwa yanayoongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Magonjwa haya yameshakuwepo kwa kipindi kirefu katika nchi zinazoendelea kutokana na mitindo ya maisha.


Magonjwa ya moyo yapo ya aina tofauti, yapo yale ya kurithiwa ambapo mtoto huzaliwa nayo, na pia yapo yale yanayotokana na maambukizi pamoja na magonjwa ambayo si ya kuambukiza.


Makala hii imejikita kuangalia dalili mbalimbali ambazo zinaweza kumaanisha kuwa mtu huyu ana tatizo la moyo. Kumbuka dalili za magonjwa ya moyo huweza kufanana na dalili za magonjwa mengine kama vile, magonjwa ya figo na ini.


Dalili za ugonjwa wa moyo kwa wanawake huwa tofauti na wanaume, mfano wanaume hupata sana maumivu ya kifua, wakati wanawake hupata dalili ya kifua kizito na kushindwa kupumua vema. Hii ndio maana dalili katika makala hii zimegawanywa kwa wanawake na wanaume na kutokana na visababishi pia halisi vya tatizo la moyo.


Dalili zisizotegemea jinsia na umri

Dalili kwa ujumla za ugonjwa wa moyo huwa ni

  • Maumivu ya kifua

  • Kubana kwa kifua

  • Kukandamizwa kwa kifua au kutohisi vema ndani ya kifua

  • Kuishiwa pumzi

  • Maumivu, udhaifu au kuhisi baridi kwenye miguu na mikono

  • Maumivu ya shingo, taya, koo na maeneo juu ya tumbo au nyuma ya mgongo


Dalili za ugonjwa wa moyo zinazosababishwa na mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi

  • Kutikisika kwa maeneo ya kifua karibu na moyo

  • Mapigo ya moyo kwenda taratibu

  • Kutohisi vema ndani ya kifua

  • Kizunguzungu

  • Kichwa kuwa chepesi

  • Kuzimia


Dalili za magonjwa ya moyo yanayosababishwa na madhaifu katika maumbile ya moyo

  • Kuwa na rangi ya bluu kwenye ngozi

  • Kuvimba kwa miguu

  • Kuvimba kwa tumbo

  • Kuvimba kwa maeneo yanayozunguka macho

  • Kuishiwa pumzi wakati wa kunyonya kwa vichanga

  • Kutoongezeka uzito vema kwa watoto vichanga

  • Kuchoka haraka wakati wa mazoezi

  • Kuishiwa pumzi kwenye shughuli ndogo tu

  • Kuvimba kwa kiwiko cha mguu, miguu na kanyagio


Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na udhaifu kwenye misuli ya moyo

  • Kupumua kwa shida wakati unataka kusimama au kutembea

  • Kuvimba kwa miguu, kiwiko cha mguu na kanyagio

  • Uchovu

  • Maopigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo

  • Kizunguzungu, hisia za kichwa chepesi na kuzimia


Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na maambukizi kwenye moyo

  • Homa

  • Kuishiwa pumzi

  • Kuvimba kwa miguu na tumbo

  • Kubadilika kwa mapigo ya moyo

  • Kikohozi kikavu

  • Harara kwenye ngozi


Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na magonjwa ya milango ya moyo

  • Uchovu

  • Kuishiwa pumzi

  • Mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo

  • Kuvimba kwa kiwiko cha mguu na miguu

  • Kuzimia


Dalili za magonjwa ya moyo kwa wanawake

  • Kutohisi vema ndani ya kifua

  • Maumivu ya kifua katikati ya kifua

  • Kuhisi kifua kama kimekandamizwa na kitu kizito

  • Maumivu au kutojihisi vema mkono wa kushoto na mabega

  • Kuishiwa pumzi bila kuw ana maumivu ya kifua

  • Kichefuchefu na kichwa kuwa chepesi

  • Kuzimia

  • Kutokwa kwa kijasho cha baridi


Dalili za ugonjwa wa moyo kwa wanaume

  • Maumivu ya kifua kama vile ya kuchana kitu

  • Kuhisi mgandamizo kwenye kifua

  • Kuhisi kifua kimejaa kw andani

  • Maumivu kwenye mkono wa kushoto, taya au nyuma ya mgongo

  • Kuishiwa pumzi

  • Kutokwa na kiijasho cha baridi

  • Kichefuchefu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Heart. Heart attack. https://www.heart.org/en/health-topics/heart-attack/warning-signs-of-a-heart-attack/heart-attack-symptoms-in-women. Imechukuliwa 12.11.2020

2.Medal news today. Signs of heart disease in men.https://www.medicalnewstoday.com/articles/322237. Imechukuliwa 12.11.2020

3.Symptoms of a heart attack. American Heart Association Go Red for Women. https://www.goredforwomen.org/en/about-heart-disease-in-women/signs-and-symptoms-in-women/symptoms-of-a-heart-attack. Imechukuliwa 12.11.2020

4.Pagidipati, N. Clinical features and diagnosis of coronary heart disease in women. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 12.11.2020

5.Heart attack symptoms. Office on Women's Health. https://www.womenshealth.gov/heart-disease-and-stroke/heart-disease/heart-attack-and-women/heart-attack-symptoms. Imechukuliwa 12.11.2020

6.Ischemic heart disease. National Heart, Lung, and Blood Institute. . https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/ischemic-heart-disease. Imechukuliwa 12.11.2020

bottom of page