Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
5 Mei 2020 17:33:32
Jicho jekundu
Jicho jekundu (Macho mekundu) ni hali ambayo sehemu ya jicho iliyo na rangi nyeupe (konjunctiva) huonekana kuwa na rangi nyekundu. Hali ya wekundu hutokea kutokana na kutanuka kwa mishipa ya damu, kutanuka huku husababishwa na hali na maambukizi mbalimbali.
Jicho jekundu linaweza kuambatana na maumivu au la. Endapo litaambatana na maumivu ni vema kumuona daktari kwa vipimo na uchunguzi. Hata hivyo jicho jekundu huweza kuathiri jicho moja au yote na mara nyingi hutokea kama mtu amekaa kwenye mwanga mdogo ,kukosa usingizi wa kutosha na matumizi ya pombe kupita kiasi.
Visababishi
Magonywa na hali
Ugonjwa wa konjanktivaitizi
Trakoma
Jeraha kwenye kornea
Glaukoma
Yuveitizi (Kuvimba kwa kuta za macho)
Pterigiamu (uvimbe ambao huanza kwenye seli za ndani ya jicho na huja kwenye kornea )
Mzio
Mazingira
Mzio kutoka kwenye hewachafu
Uchafuzi wa hali ya hewa
Moshi
Hewa kavu
Vumbi
Kupita mazingira ya kemikali
Kukaa kwenye jua sana
Kama sababu ya kuwa na macho mekundu ni kutokana na sababu hizo zilizotajwa hapo juu, unapaswa kujikinga na sababu zinazokingika.
Dalili za jicho jekundu
Dalili za mtu mwenye jicho jekundu ni pamoja na;
Jicho moja au yote kuwa na rangi nyekundu
Huweza kutoa machozi
Huweza kuwa jicho kavu lisilotoa machozi
Maumivu ya kichwa
Muwasho wa jicho
Kuhisi hali ya mchanga kwenye macho
Maumivu ya macho
Kutokuona vizuri
Vipimo
Kama kuna uchafu wowote unatoka kwenye jicho mfano usaha na maji yanayotoka yanapaswa kupelekwa maabara kwa ajili ya kupimwa.
Matibabu
Kama unatokwa na usaha unapaswa kupata dawa za antibayotiki
Kama ni mzio daktari wako atakupa dawa za kuzuia mzio
Kumbuka
Kila sababu inayosababisha macho kuwa mekundu inapaswa kutibiwa yenyewe kwa kujitegemea.
Dalili hii ya jicho jekundu endapo haitatibiwa mapema endapo inasababishwa na sababu ya hatari inaweza kupelekea mtu kupoteza uwezo wa kuona.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 04:52:37
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.All About Vision.https://www.allaboutvision.com/conditions/red-eyes.htm Imechukuliwa 5/5/2020
2. Red Eyes Causes. MayoClinic. https://www.mayoclinic.org/symptoms/red-eye/basics/causes/sym-20050748 . Imechukuliwa 5/5/2020
3.Red Eyes HealthLine. https://www.healthline.com/health/eye-redness. Imechukuliwa 5/5/2020
4.WebMd.Red Eyes. https://www.webmd.com/eye-health/why-eyes-red#1. Imechukuliwa 5/5/2020