Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
6 Mei 2020, 10:25:06
Komahedhi
Mwanamke mwenye umri kati ya miaka 45 hadi 55 huwa kwenye koma hedhi kama ameacha kuona damu ya mwezi kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo, pasipo kuwa na ujauzito au magonjwa yanayoathiri hedhi. Ukiingia koma hedhi kabla ya umri wa miaka 40, wasiliana na daktari kwa uchunguzi na tiba. Koma hedhi hutanguliwa mara nyingi na kukoma kwa uzalishaji wa mayai na kupoteza uwezo wa kupata ujauzito.
Hatua za kukoma kwa hedhi
Kipindi kabla ya kukoma kwa hedhi- Hutokea kabla ya kufikisha umri wa miaka 40 huambatana na dalili mbalimbali
Kipindi cha kuelekea koma hedhi- Kipindi hiki huambatana na dalili za kufikia mwisho wa hedhi kukoma
Koma hedhi- Hiki ni kipindi cha umri wa miaka 45 hadi 55 wastani wake ni miaka 50
Kipindi baada ya koma hedhi- Hiki ni kipindi baada ya hedhi kukoma na kutuoina angalau kwa miezi 12 mfululizo
Visababishi
Koma hedhi hutokea kama ovari imekoma kuzalisha mayai na hakuna homoni kukosekana kwa homon zinazosisimua ovari kuzalisha mayai hayo.
Visababishi vya komahedhi kabla ya wakati
Komahedhi kabla ya wakati huweza tokea kwenye umri wowote ule kabla ya kufikisha umri wa miaka 45 na mara nyingi hakuna sababu inayofahamika kuhusika.
Baadhi ya sababu zinazochangia kupata koma hedhi kabla ya wakati ni;
Matibabu ya upasuaji wa kuondoa ovari
Baadhi ya matibabu ya saratani ya titi
Matumizi ya dawa za saratani (kemotherap)
Matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi
Kuwa na sindromu ya Down's
Kuwa na ugonjwa wa Addison's
Umri wa koma hedhi
Koma hedhi huweza anza taratibu kwa kipindi cha miezi kadhaa au kwa miaka kadhaa kabla ya kusimama kabisa. Unaweza kuwa na vipinid vya kutoona hedhi na kurejea kisha kukoma kabisa.
Koma hedhi hedhi asili mara nyingi hutokea kwa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 45 hadi 55, wastani wa ukiwa miaka 51
Koma hedhi inaweza tokea kabla ya umri wa miaka 45?
Ndio koma hedhi inaweza kutokea kwa baadhi ya wanawake walio chini ya umri wa miaka 40. Tafiti zinaonyesha, mwamake 1 kati 100 hukomahedhi kabla ya kufikia umri wa miaka 40 na hii hufahamika komahedhi kabla ya wakati. Visababishi vya aina hii ya komahedhi mara nyingi huwa havifahamika lakini baadhi ya sababu zimeorodheshwa kwenye aya zinazofuata.
Dalili za koma hedhi
Kuongezeka kwa lehemu kwenye damu, hii humpelekea mwanamke huyu kuwa na hatari ya kupata magonjwa ya moyo
Mifupa kuwa dhaifu kuweza kuvunjika kwa uraisi, hii ni kutokana na hali ya kuwa na homoni kiasi kudogo cha Estrogen
Mfumo wa umeng’enyaji chakula kwenda taratibu na mara nyingi hupelekea kukosa choo au kupata choo kigumu
Kukojoa mara kwa mara kutokana na mrija wa mkojo na mfuko wa mkojo kuwa mfupi na mwembamba kutokana na upungufu wa homon Estrogen
Kusinyaa na kupungua umbo la ovari
Kusinyaa kwa mirija wa fallopio
Kusinyaa kwa mfuko wa uzazi
Kusinyaa kwa kuta za uke uke huwa na kupata hali ya akaline
Kusinyaa kwa maeneo ya siri ( uke na mashavu yake)
Kusinyaa kwa matiti na kupungua umbile au kulala
Ngozi ya mwili huanza kusinyaa na kutokuvutia
Kuongezeka kwa Uzito
Kupoteza nywele maeneo mbalimbali ya mwili
Sauti huanza kuwa ndogo
Kutokwa na jasho wakati wa usiku
Kuhisi hali ya joto, huanzia kwenye uso na ghafla husambaa kwenda kwenye shingo na mwili mzima
Maumiu ya kichwa yamara kwa mara
Mwili kuchoka
Kuwa na hali ya huzuni
Kukosa usingizi
Kukosa hamu ya mapenzi
Uke kuwa mkavu
Kumbuka
Dalili za mapema za komahedhi hutokea kabla ya miaka 40
Wakati gani wa kuonana na daktari?
Unapswa kuwasiliana na daktari wako kama utaona dalili za hedhi kabla ya kufikisha umri wa miaka 45 au dalili za komahedhi zinakusumbua kiasi cha kutoweza ishi vema.
Daktari mbali na kuthibitisha kwa dalili, atashibitisha kuwa umeingia komahedhi kwa kipimo cha kiwango cha homon kwenye damu kama komahedhi imetokea kabla ya kuingia umri wa miaka 45
Matibabu
Matibabu huhusisha tiba ya dawa za homoni ziada kwa ajili ya kupunguza dalili za koma hedhi na kuzuia mifupa kuvunjika
Dawa mchanganyiko wa Estrogen na progesterone hutolewa kwa pamoja, Estrogen endapo ikatolewa peke yake kwa mama mfuko wa uzazi huweza kupelekea kukua na kupelekea kansa ya kizazi
Estrogen peke ake hutolewa kwa kwa wanawake ambapo vizazi vyao vilikwisha kutolewa
Tiba saikolojia na kujitambua
Matibabu mengine
Zipo njia za kufanya endapo mama hataweza kupata homoni za mbadala
Kufanya mazoezi
Kula vyakula vyenye protini kwa wingi
Kupewa vidongr madini ya ziada ya kalisiamu
Kupewa vitamin D ya ziada
Kuacha kuvuta sigara na pombe
Madhara
Matumizi ya homoni za ziada katika kutibu dalili za komahedhu huongeza hatari ya;
Kupata saratani ya kizazi
Kupata saratani ya matiti
Kupata magonjwa ya moyo
Magonjwa ya kusahau
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021, 04:52:43
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Web.Md.Menopause.https://www.webmd.com/menopause/guide/menopause-symptoms-types. Imechukuliwa 10/4/2020
2.Health.Line.Today.Menopause.https://www.healthline.com/health/menopause.Imechukuliwa 10/4/2020
3.Menopause. National Institute on Aging. http://www.nia.nih.gov/health/publication/menopause. Imechukuliwa 10.04.2020
4.Casper RF, et al. Clinical manifestations and diagnosis of menopause. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
5.Longo DL, et al., eds. Menopause and postmenopausal hormone therapy. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 10.04.2020
6.Nelson LM, et al. Clinical manifestation and evaluation of spontaneous primary ovarian insufficiency (premature ovarian failure). https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
7.Menopausal symptoms and complementary health practices. National Center for Complementary and Alternative Medicine. http://nccam.nih.gov/health/menopause/menopausesymptoms. Imechukuliwa 10.04.2020
8.Medical.New.Today.Menopause.https://www.medicalnewstoday.com/articles/155651.Imechukuliwa 10/4/2020
9.Dc Dutta Textbook Gynaecology ISBN 978-93-5152-068-9 written by Hiralal Konar Ukurasa wa 57-60