Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
11 Desemba 2020 14:02:45
Kuhisi mapigo ya moyo
Hisia za mapigo ya moyo huitwa kitiba kwa jina la 'palpitation', hii ni hali ya kuhisi moyo unakwenda taratibu au kwa kasi zaidi ya kawaida. Hisia za mapigo ya moyo huweza kusababishwa na mambo ya kawaida ambayo huhitaji kuwa na hofu nayo au kumaanisha tatizo la moyo linalohitaji kufanyiwa uchunguzi wa haraka, hata hivyo mara nyingi hisia za mapigo ya moyo huwa hazisababishwi na mambo ya hatari.
Katika makala hii utajifunza kuhusu visababishi vya kuhisi mapigo ya moyo na namna ya kukabiliana nayo.
Dalili
Dalili za kuhisi mapigo ya moyo huwa pamoja na;
Hisia za pigo moja la moyo kuruka
Hisia za pigo la moyo kuongezeka
Hisia za moyo kwenda taratibu
Hisia za moyo kugonga katika kuta za kifua
Kuhisi moyo unakwenda kasi kuliko kawaida
Kuhisi mapigo ya moyo kwenye maeneo ya koo, shingo na kifuani
Wakati gani wa kumwona daktari
Endapo mapigo ya moyo yanaenda kasi au taratibu kwa dakika chache na kupotea, huna haja ya kuonana na daktari. Endapo hali ya mapigo ya moyo kwenda kasi au taratibu imetokea mara kwa mara ni vema ukaonana na daktari kwa uchunguzi Zaidi. Hata hivyo unapaswa kumwona daktari wako haraka endapo mapigo ya moyo yanaambatana na dalili zifuatazo;
Maumivu ya kifua au kupata bughudha ndani ya kifua
Kuzimia
Kizunguzungu kikali
Kuishiwa pumzi
Kuwa na tatizo la moyo
Historia ya mwana familia wa damu moja kufa ghafla kwa sababu ya tatizo la moyo
Hisia za mapigo ya moyo wakati unafanya mazoezi haswa kuzimia
Visababishi
Mara nyingi kisababishi huwa hakifahamiki, hata hivyo baadhi ya vitu vinavyyoweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi ni;
Msongo wa mawazo
Hisia kali kama za kupaniki, shauku kali n.k
Mazoezi makali
Magonjwa
Matumizi ya dawa za kuchangamsha mwili kama kahawa, cocaine, amphetamine na dawa za kutibu homa ya mafua zenye pseudoephedrine
Homa
Mabadiliko ya homoni mwilini haswa wakati wa kuona damu ya mwezi, ujauzito, au kipindi cha komahedhi
Kuwa na kiwango cha chini cha homoni thyroid
Kutopata usingizi wa kutosha
Kuishiwa maji mwilini
Madhaifu katika electrolyte mwilini
Kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu
Upungufu wa damu mwilini
Mshituko wa moyo
Tatizo la arrhythmia
Apnea
Kushuka kwa shinikizo la damu wakati wa kusimama(orthostatic hypotension)
Vihatarishi
Vitu vifuatavyo vinaweza kupelekea ukapata tatizo la kuhisi mapigo ya moyo
Kuwa katika kipindi kirefu cha msongo wa mawazo
Kuwa na ugonjwa wa shauku au kutaharuki
Kuwa na ujauzito
Kuwa unatumia dawa za kushitua mfumo wa sympathetic kama albuterol, amphetamines, cocaine, dobutamine, epinephrine, ephedrine, isoproterenol, norepinephrine, and theophylline
Kuwa na magonjwa ya moyo mfano, tundu kwenye moyo, historia ya kupata mshituko wa moyo au kufanyiwa upasuaji wa moyo
Kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya thyroid kwenye damu (hypethyroidism)
Vipimo
Mara nyingi endapo kuna uhajua wa kufanya kipimo, kipimo kinachoanza kufanyika ili kusoma shughuli za moyo ni kipimo cha ECG. Baada ya kipimo hiki daktari ataamua kufanya vipimo vingine vya kutambua tatizo ambalo limeonekana kwenye kipimo hiki cha awali. Vipimo vingine ni pamoja na vipimo vya damu na kipimo cha echocardiography, MRI au PET scan.
Matibabu
Matibabu ya kuhisi mapigo ya moyo hutegemea kisababishi. ULY CLINIC inakushauri usome zaidi kuhusu kisababishi ulichokitambua ili kufahamu kuhusu matibabu yake.
Madhara
Madhara ya kuhisi mapigo ya moyo ni;
Kuzimia- endapo shinikizo la damu litashuka utazimia
Mshituko wa moyo- moyo kusimama kufanya kazi, hii huweza kupeekea kifyo cha ghafla
Kiharusi(stroke)
Kuferi kwa moyo-endapo tatizo limedumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi
Kinga
Endapo unapata hisia za mapigo ya moyo, wakati mwingine inaweza isiwe lazima kupata matibabu endapo kisababishi ni mambo yanayohusisha mtindo wa maisha. Ili kujikinga na kuhisi moyo kwenda kasi unaweza kufanya au kufuata vitu vifuatavyo;
Kama kuna dawa inayosababisha mapigo ya moyo kwenda kasi, hakikisha unawasiliana na daktari wako ili akufanyie uchugnuzi na kukubadilishia dawa
Endapo una msongo wa mawazo au tatizo la shauku kali, hakikisha unafanya mazoezi ya kutuliza akili an mwili wako(yoga)
Fanya mazoezi kwa mpangilio maalumu
Fanya uchugnuzi wa kufahamu ni vitu gani vinavyokupelekea mapigo ya moyo kwenda kasi kwa kurekodi unachokila, kisha viepuke
Kula mlo kamili na kila siku
Punguza kiwango cha pombe unachokunywa kwa kunyw akiwango kinachoshauriwa kitaalamu
Usivute sigara au kutumia mazao yanayotokana na tumbaku
Dhibiti shinikizo la damu kwa kutumia dawa na matibabu ya chakula
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Zimetbaum PJ. Overview of palpitations in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. imechukuliwa 11.12.2020
2. Heart palpitations. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/hpl#. Imechukuliwa 11.12.2020
3. Heart palpitations and ectopic beats. nhs.uk/conditions/Heartpalpitations/Pages/Introduction.aspx. Imechukuliwa 11.12.2020
4. Skipping a beat the surprise of heart palpitations.health.harvard.edu/heart-disease-overview/skipping-a-beat--the-surprise-of-palpitations. Imechukuliwa 11.12.2020
5. Palpitations. https://www.msdmanuals.com/professional/cardiovascular-disorders/symptoms-of-cardiovascular-disorders/palpitations. Imechukuliwa 11.12.2020
6. Amandeep Goyal; etal. Palpitations. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK436016/
7. Benefits of an early management of palpitations. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6076186/. Imechukuliwa 11.12.2020
8. David M. Mirvis. Palpitations. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK202/. Imechukuliwa 11.12.2020