top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter B, MD

11 Desemba 2020 15:01:27

Moyo kwenda kasi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Moyo kwenda kasi

Moyo kwenda kasi kitiba hufahamika kama tachycardia, hii ni hali ya kuhisi moyo unakwenda kwa kasi Zaidi ya kawaida. Kwa kawaida mapigo ya moyo huhesabiwa kwa kuhesabu midundo ya mishipa ya damu au kuhesabu midundo ya moyo. Endapo midundo ya moyo imezidi kiwango cha midundo 100 kwa dakika moja(100b/min) mtu husemekana kuwa ana tatizo la tachycardia.


Baadhi ya nyakati mapigo ya moyo kwenda kasi huweza kusababishwa na mambo ya kawaida mfano mazoezi, ugonjwa au mshituko wa kawaida kama unapopokea habari mbaya n.k hata hivyo baadhi ya wakati, moyo kwenda kasi huweza kusababishwa na sababu zinazohitaji ufanyiwe uchunguzi wa haraka ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kama mshituko wa moyo, kuferi kwa moyo na kiharusi.


Dalili


Baadhi ya watu wenye tatizo hili huwa hawana dalili zozote zile, hata hivyo endapo zitaonekana dalili hizo huwa ni;


  • Kuishiwa pumzi

  • Kizunguzungu

  • Kuongezeka kwa mdundo wa mishipa ya damu

  • Kuhisi mapigo ya moyo

  • Maumivu ya kifua

  • Kuzimia


Wakati gani wa kumwona daktari?


Endapo mapigo ya moyo yanaenda kasi kwa dakika chache na kupotea, huna haja ya kuonana na daktari isipokuwa endapo hali ya mapigo ya moyo kwenda kasi inajitokeza mara kwa mara. Hata hivyo unapaswa kumwona daktari wako haraka endapo mapigo ya moyo yanaambatana na dalili zifuatazo;


  • Maumivu ya kifua au kupata bughudha ndani ya kifua

  • Kuzimia

  • Kizunguzungu kikali

  • Kuishiwa pumzi

  • Kuwa na tatizo la moyo


Visababishi


Baadhi ya vitu vinavyyoweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi ni;


  • Msongo wa mawazo

  • Hisia kali kama za kupaniki, shauku kali n.k

  • Mazoezi makali

  • Magonjwa

  • Matumizi ya dawa za kuchangamsha mwili kama kahawa, cocaine, amphetamine na dawa za kutibu homa ya mafua zenye pseudoephedrine

  • Homa

  • Mabadiliko ya homoni mwilini haswa wakati wa kuona damu ya mwezi, ujauzito, au kipindi cha komahedhi

  • Tatizo la hypothyroidism au hypathyroidism

  • Kutopata usingizi wa kutosha

  • Kuishiwa maji mwilini

  • Madhaifu katika electrolyte mwilini

  • Kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu

  • Upungufu wa damu mwilini

  • Mshituko wa moyo

  • Tatizo la arrhythmia

  • Apnea

  • Kushuka kwa shinikizo la damu wakati wa kusimama(orthostatic hypotension)


Vihatarishi


Vitu vifuatavyo vinaweza kupelekea ukapata tatizo la mapigo ya moyo kwenda mbio


  • Kuwa katika kipindi kirefu cha msongo wa mawazo

  • Kuwa na ugonjwa wa shauku au kutaharuki

  • Kuwa na ujauzito

  • Kutumia dawa za kushitua mfumo wa sympathetic kama albuterol, amphetamines, cocaine, dobutamine, epinephrine, ephedrine, isoproterenol, norepinephrine, and theophylline

  • Kuwa na magonjwa ya moyo mfano, tundu kwenye moyo, historia ya kupata mshituko wa moyo au kufanyiwa upasuaji wa moyo

  • Kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya thyroid kwenye damu (hypethyroidism)


Madhara


Madhara yanayoweza kutokea kutokana na tatizo hili ni;


  • Kuganda kwa damu- huweza kupelekea kupata kiharusi na mshituko wa moyo

  • Moyo kuferi kufanya kazi

  • Kuzimia mara kwa mara na kupoteza fahamu

  • Kifo cha ghafla


Vipimo


Mara nyingi endapo kuna uhajua wa kufanya kipimo, kipimo cha kwanza kinachoanza kufanyika ili kusoma shughuli za moyo ni kipimo cha ECG. Baada ya kipimo hiki daktari ataamua kufanya vipimo vingine vya kutambua tatizo ambalo limeonekana kwenye kipimo hiki cha awali. Vipimo vingine ni pamoja na vipimo vya damu na kipimo cha echocardiography, MRI au PET scan.


Matibabu


Matibabu ya mapigo ya moyo kwenda kasi hutegemea kisababishi. ULY CLINIC inakushauri usome zaidi kuhusu kisababishi ulichokitambua baada ya kusoma makala hii kwa uelewa zaidi kuhusu matibabu


Kinga


Ili kujikinga na tatizo la mapigo ya moyo kwenda kasi, ni vema ukazingatia kanuni za kufanya moyo wako uwe na afya njema kwa kufanya mambo yafuatayo;


  • Fanya mazoezi yenye mpangilio maalumu mara tatu au nne kwa wiki kwa kipindi cha nusu saa na kuendelea

  • Kula mlo kamili na vyakula ambavyo ni vizuri kwa afya ya moyo, mfano vyakula vyenye mafuta kidogo, vyakula vya nafaka zisizokobolewa, mboga za majani na matunda kwa wingi

  • Kuwa na uzito wa kiafya. Punguza uzito endapo una tatizo la obezity

  • Hakikisha kiwango cha kolestro kwenye damu kipo katika kiwango kinachoshauriwa kiafya

  • Acha kuvuta sigara au mazao yatokanayo na tumbaku

  • Kunywa pombe kwa kiasi kinachoshauriwa kiafya endapo wewe ni mtumiaji wa kilevi

  • Usitumie dawa za kulevya au za kuamsha mfumo wa symphathetic

  • Unapotumia dawa, zitumie kwa umakini, dawa ambazo zinakupelekea mapigo ya moyo kwenda kasi ziache baada ya kupata ushauri kutoka kwa daktari wako

  • Jizuie kutumia kahawa mara kwa mara

  • Dhibiti msongo wa mawazo

  • Fanya uchunguzi wa afya ya moyo wako

  • Pata matibabu ya magonjwa ya moyo na hudhuria kliniki yako na kliniki za elimu

  • Penda kusoma zaidi kuhusu makala mbalimbali za kiafya ili kuwa na uelewa zaidi wa kanuni za kiafya

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:12

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Crawford MH, ed. Ventricular tachycardia. In: Current Diagnosis & Treatment: Cardiology. 5th ed. McGraw-Hill Education; 2017. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 11.12.2020
2. Homoud MK, et al. Sinus tachycardia: Evaluation and management. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 11.12.2020
3. Overview of arrhythmias. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/cardiovascular_disorders/arrhythmias_and_conduction_disorders/overview_of_arrhythmias.html?qt=arrhythmia&alt=sh. Imechukuliwa 11.12.2020
4. Prevention & treatment of arrhythmia. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/Arrhythmia/PreventionTreatmentofArrhythmia/Prevention-Treatment-of-Arrhythmia_UCM_002026_Article.jsp. Imechukuliwa 11.12.2020
5. What is an arrhythmia? National Heart, Lung, and Blood Institute. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/arr/. Imechukuliwa 11.12.2020
6. What is catheter ablation? National Heart, Lung, and Blood Institute. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/ablation/. Imechukuliwa 11.12.2020
7. Zipes DP, et al., eds. Diagnosis of cardiac arrhythmias. In: Cardiac Electrophysiology: From Cell to Bedside. 7th ed. Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 11.12.2020

bottom of page