Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
28 Machi 2020, 07:49:36
Obeziti
Obeziti ni ugonjwa unaohusisha kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta mwilini. Ugonjwa huu si tu unaathiri mwonekano wa mtu, bali huongeza hatari ya kupata magojnwa mengine kama vile magonjwa a moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani aina fulani.
Kutonana na sababu nyingi za kimazingira na kurithi , baadhi ya watu wanashindwa kupambana na tatizo hili.
Hata hivyo mabadiliko ya mtindo wa Maisha, kufanya mazoezi na kutumia dawa za kuandikiwa na daktari husaidia kupunguza uzito na kukukinga au kukuzuia kupata magonjwa yatokanayo na obeziti. Uzito kupita kiasi imekuwa ni shida sana katika jamii tunayoishi kwa sasa kutokana na kubadilika kwa mtindo wa maisha na kutofanya kazi za kutoa jasho.
Visababishi
Kula vyakula visivyo vya kiafya
Vyakula vyenye nishati nyingi (mfano wanga), visivyo na matunda na mboga za majani, vyakula vyenye mafuta, vinywaji kama soda na juisi za viwandani. Pombe na soda huongeza uzito kwa kiasi kikubwa bila mtu kujua kwa sababu huwa na nishati kwa kiasi kikubwa na huonekana kutoshibisha pia
Kutoushughulisha mwili
Endapo unaishi Maisha ya kukaa au unafanya kazi za kukaa ofisini bila kuwa na ratiba ya mazoezi endelevu una hatari ya kupata tatizo la obeziti.
Magonjwa na dawa
Magonjwa kama ugonjwa wa sindromu ya Prader-Will , 'sindrome ya cushing', athraitizi na gauti pia yanaweza kupelekea kushindwa kuushughulisha mwili na kukupa hatari ya kuongezeka zaidi. Baadhi ya dawa zinazoongeza uzito ni kama dawa jamii ya antidepressant, ant-seizure, dawa za kisukari, dawa jamii ya antsaikotiki, steroidi na beta bloka.
Umri kuongezeka
Obeziti inaweza kutokea kwenye umri wowote ule iwe mtoto au mtu mzima. Hata hivyo watu hupunguza au kuacha kujishughulisha kwa kazi za kuuchangamsha mwili kwa jinsi umri unavyoongezeka. Uzee pia huambatana na kupungua ukubwa wa misuli. Kuisha kwa misuli hupunguza matumizi ya sukari mwilini na hivyo sukari hii hutunzwa kama Mafuta. Kama usipodhibiti unachokula basi ni rahisi kuongeeka uzito mara dufu zaidi na kushindwa kupungua kirahisi.
Visababishi vingine
Ujauzito
Mara baada ya kujifungua, mama huongezeka uzito kutokana na mabadiliko ya homoni, mama akishindwa kudhibiti anachokula au asiponyonyesha mtoto ana hatari kubwa ya kuwa na tatizo la obeziti.
Kutopata usingizi wa kutosha au kulala muda mrefu
Kutopata usingizi wa kutosha au kulala sana huleta mabadiliko ya homoni mwilini na baadhi ya watu hupata hamu ya kula, hivyo kupenda kula vyakula vyenye nguvu nyingi na kusababisha kuongezeka uzito.
Msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo huathiri hali ya moyo wa mtu na huweza kuchangia kupata obeziti.
Kuferi kwa programu ya kupunguza uzito
ndapo wakati uliopita ulikuwa kwenye programu ya kupunguza uzito na ukaishia njiani, uzito utajirudia mara dufu. Ni vema ukaendelea kudhibiti uzito wako endapo umeamua kupunguza uzito. Soma Zaidi kuhusu mazoezi ya kupunguza uzito kwenye mada ya chakula na mazoezi kwenye tovuti hii.
Aina
Obeziti imegawanyika katika sehemu kuu mbili kutokana na sehemu ya mwili inayoathiriwa mwili ambazo ni
Obeziti ya kiwiliwili: Hii aina huambatana zaidi na magonjwa ya Kiharusi ,mishipa ya damu na baadhi ya saratani: Aina hii ni hatari zaidi
Obeziti ya chini ya kiwiliwili: Kama kwenye maeneo ya nyonga ,Matako na mapaja- Aina hii haimbatani na magonjwa sana kama aina ya kwanza.
Madhara
Obeziti huambatana na magonjwa yafuatayo:
Magonjwa ya mishipa ya damu na mshituko wa moyo
Magonjwa ya moyo
Shinikizo la juu la damu(presha)
Kisukari
Saratani kwa wanawake kama saratani ya matiti na utumbo mkubwa na kwa wanaume kama
saratani ya Tezi dume na utumbo mkubwa
Kiharusi
Matatizo ya kupumua
Magonjwa ya mfumo wa uzazi
Matatizo ya hedhi
Matatizo ya homoni mwilini
Kwa wanaume wengi wenye uzito kupita kiasi huwa na shida ya kupungua uzalishwaji wa homoni ya testosteroni.
Magonjwa mengi ambayo husababishwa na uzito kupita kiasi hupelekea vifo vinavyoweza kuzuilika
Unawezaje kujua kuwa una obeziti ?
Njia nzuri ya kuweza kujua ni kupima BMI yako
Je BMI ni nini?
Wanariadhana wanaojenga misuli hawatakiwi kutumia kipimo cha BMI kama njia ya kupima uimara BMI kwa sababu huwa wanamisuli mingi kuliko mafuta.
Pia kwa wamama wajawazito BMI huweza kuonyesha majibu ya uongo kutokana na mama kuwa na uzito wa mtoto.
BMI na makundi yake
Kuanzia 19-24.9: Hili kundi haliko kwenye hatari ya kiafya
Kuanzia 25-29.9:Ni uzito kupita kiasi pia huwa na hatari ya kawaida katika afya
Kuanzia 30 na Kuendelea :Ni uzito usio wa kawaida na huambatana na hatari zaidi ya kupata magonjwa
Namna ya kujikinga na obeziti
Fanya mambo yafuatayo kwa ushauri kutoka kwa daktari wako ili kujizuia na tatizo la obeziti na mdahra yake;
Kula vyakula vyenye mboga za majani na matunda kwa wingi kalori kidogo, Mafuta kiasi au visivyo na mafuta.
Kufanya mazoezi katika ratiba maalumu angalau mara 3 au 4 kwa wiki.
Kuepuka kunywa pombe kwa wingi maana imetengenezwa kwa wanga na vyakula vyenye nguvu nyingi kama soda na vinywaji wa energetic.
Epuka mambo yanayoweza kukuletea msongo wa mawazo ,pia pata muda wa kutosha wa kulala wakati wa usiku angalau masaa 7 hadi 8 kwa siku.
Kunywa maji ya kutosha angalau glasi nane kwa siku..
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1)https://www.healthline.com/nutrition/low-calorie-foods
2)Harrison Principles of Internal Medicine Ukurasa wa 421-425
3)Encyclopedia of Foods a guide to health Nutrition, Ukurasa wa 47-52
4)https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/obesity/symptoms-causes/syc-20375742
5)https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/obesity-and-overweight
6)Jameson JL, et al., eds. Evaluation and management of obesity. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 28.03.2020
7)Usatine RP, et al., eds. Obesity. In: The Color Atlas and Synopsis of Family Medicine. 3rd ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2019. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 28.03.2020
8)McKean SC, et al., eds. Surgical management of obesity. In: Principles and Practice of Hospital Medicine. 2nd ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2017. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 28.03.2020
9)Perreault L, et al. Obesity in adults: Prevalence, screening, and evaluation. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.03.2020
10)Perreault L, et al. Obesity in adults: Overview of management. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.03.2020