Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
4 Mei 2020, 18:30:22
Ulimi uliopasuka
Ulimi uliopasuka na kuwa na mifereji (ulimi kuchanika) ni tatizo linalojulikana sana, tatizo hili hutokana na matatizo asili ya kiuumbaji na hakuna kisababishi kinachofahamika kusababisha tatizo hili. Hata hivyo tatizo hili si saratani wala halina hatari ya kuwa saratani.
Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kwamba, ulimi uliopasuka na kuwa na mifereji Pamoja na tatizo la ulimi jiografia hurithiwa na huweza kuambatana pia na tatizo la soriasisi.
Mwathirika wa ulimi uliopasuka, ulimi wake huwa na mifereji mingi sehemu ya juu ya ulimi na kuwa na mwonekano jinsi Ngozi ya pumbu ilivyo. Mipasuko inaweza kutofautiana kwa upana,kina na idadi kutoka mtu mmoja na mwingine na mara nyingi huwa na mpangilio maalumu. Tatizo hili huwa halina dalili yoyote, hata hivyo uchafu wa chakula, vimelea na fangasi wanaweza kukaa kwenye kina cha mipasuko hii na kuleta uchokozi kwenye uimi na mtu kupata dalili za maumivu ya ulimi au kubadilika kwa ulimi.
Tatizo la ulimi uliopasuka hutokea kwa asilimia 0.5 hadi 5 ya watu
Ulimi uliopasuka unaweza kutokea Pamoja na tatizo jingine la ulimi ramani, ikitokea kwa Pamoja hali hii huwa na sifa za kuambatana na sindromu ya downs na sindromu ya Melkersso-Rosenthal.
Magonjwa mengine yanayoweza kusababisha hali ya ulimi kupasuka ni sindromu ya sjongre’s na kaswende ya intestisho glositizi.
Je unahitaji matibabu ya tatizo hili?
Matibabu hayahitajiki kwa kuwa hali hii si ugonjwa na tatizo hili halidhuru wala kuleta madhara yoyote, hata hivyo endapo utakuwa na dalili ambatwa kama vile maambukizi kwenye ulimi au ulimi kubadilika rangi utahitaji kufanyiwa uhunguzi wa kitaalamu na kupewa matibabu. Matibabu haya hayawezi kuondoa tatizo la ulimi kupasuka.
Nini cha kufanya endapo una ulimi uliopasuka (kuchanika)?
Unashauriwa kufanya usafi wa kinywa hako ikiwa pamoja na kupiga mswaki kwa dawa ili kuondoa uchafu wote kutoka kwenye mipasuko. Kusafisha kinywa na ulimi kutakusaidia kuepuka maambukizi kwenye kinywani ambayo yanaweza kuambatana na maumivu ya ulimi na harufu mbaya ya kinywa. Dawa mbalimbali za kusafisha ulimi zinapatikana na ni vema ukatumia kwa afya ya kinywa chako.
Daktari wa meno anaweza kukushauri namna ya kusafisha kinywa chako na kuepuka maambukizi ya kinywa.
Majina mengine ya tatizo la ulimi kupasuka
Ulimi uliopasuka
Ulimi plikata
Ulimi pumbu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021, 04:53:39
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Science direct. https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S0377123717301120?via%3Dihub. Imechukuliwa 04.05.2020
2.Color Atlas of Oral Diseases by George Laskaris, D. D. S. , M. D., toleo la 2 1991. ISBN 3-13-717002-8
3.NIH. Psoriasis. https://rarediseases.info.nih.gov/diseases/12813/pustular-psoriasis. Imechukuliwa 04.05.2020
4. AAOM. Fissured tongue.https://www.aaom.com/fissured-tongue.Imechukuliwa 04.05.2020