top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

24 Aprili 2025, 13:42:57

Dalili za gono kwa mwanamke
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za gono kwa mwanamke

Dalili za gono kwa wanawake

Dalili za gono au gonorrhea (hufahamika pia kama gonorea au kisonono) kwa wanawake na wanaume huwa hazina utofauti mkubwa isipokuwa kuchelewa kuonekana kwa wanawake.


Tafiti zinaonyesha ni asilimia 20 hadi 50 tu ya wanawake walioambukizwa gono huwa wanaonyesha dalili. Hata hivyo dalili za gono kwa wanaume huonekana haraka. Soma zaidi kuhusu dalili za gono kwa wanaume sehemu nyingine ya tovuti hii.


Dalili hizo hizo ni zipi?

Endapo dalili za gono kwa wanawake zitatokea, zifuatazo huwa miongoni mwa dalili;


  • Kutoka ute, usaha au maji machafu ukeni

  • Kutokwa na ute wenye harufu kali ukeni

  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

  • Kutokwa na ute wenye rangi ya njano, kijani au nyingine tofauti na kawaida ukeni


Matibabu ya gono kwa wanawake

Licha ya kuchelewa kutokea na kuwa na utofauti mdogo, matibabu ya gono hususisha matumizi ya dawa za antibiotiki zinazolenga kuua vimelea vya magonjwa yote ya zinaa endapo yataonekana kwenye vipimo ambayo ni kisonono, pangusa, trikomoniasisi, kaswende, chunjua na herpes. Orodha ya dawa za gono zinapatikana katika makala ya 'dawa za gono' au kwa kubofya hapa. 


Majina mengine ya dalili za gono

Dalili za gono hufahamika na wagonjwa kwa majina ya 'dalili za kisonono', 'kutokwa usaha kwenye uume', kutokwa uchafu unaonuka ukeni,'kutokwa uchafu rangi ya njano au kijani au kahawia sehemu za siri' na 'ugonjwa wa zinaa'


Wapi utapata maelezo zaidi kuhusi gono kwa wanawake?

Kwa maelezo zaidi kuhusu gono na dalili za gono au 'dalili za kisonono' ingia kwa kubofya hapa 


Mambo muhimu kufahamu kukumbuka kuhusu dalili za gono kwa wanawake


Dalili za gono zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya zinaa, hakikisha siku zote unawasiliana na daktari wako kabla ya kujipa ugonjwa na kufanya matibabu pasipo ushauri wa daktari wako.


Wapi unaweza kupata msaada zaidi?

Endapo una maswali zaidi, wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba.


Waweza wasiliana pia na daktari wa ULY CLINIC moja kwa moja kupitia kitufe cha 'mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

24 Aprili 2025, 13:42:57

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. ULYCLINIC. Dalili za gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono%28kisonono%29. Imechukuliwa 02.07.2021

2. ULY CLINIC. Dawa za gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 02.07.2021

3. NHS. STIs. https://www.nhs.uk/conditions/sexually-transmitted-infections-stis/. Imechukuliwa 02.07.2021

4. ULY CLINIC. rangi ya ute ukeni na maana yake kiafya. https://www.ulyclinic.com/post/rangi-ya-majimaji-ukeni-na-maana-zake-kiafya-uly-clinic. Imechukuliwa 02.07.2021

bottom of page