Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter Mangwella, MD
3 Desemba 2024, 13:41:21
Dalili za gono kwa mwanaume
Utangulizi
Gono ni ugonjwa wa zinaa unaojitokeza sana hasa kwa vijana, ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya ngono na mwenza mwenye maambukizi, inaweza kuwa ngono ya uume na uke, uume na njia ya haja kubwa au ngono ya mdomo. Pia mama mwenye maaambukizi anaweza kumuambukiza mtoto wakati wa kuzaliwa.
Mwanume anaweza kuwa na gono na akaonesha dalili au asioneshe dalili yoyote. Endapo ataonesha dalili huwa za wastani na huweza kuchanganywa na dalili za magonjwa mengine mfano UTI.
Je, ni zipi dalili za gono kwa mwanaume?
Kama ilivyoainishwa hapo awali, mwanaume anaweza kuwa na gono na akaonesha au asuoneshe dalili zozote. Endapo ataonesha dalili basi dalili hizo zitaonekana kulingana na sehemu iliyoathirika kama ifuatayo;
Gono inayoathiri via vya uzazi
Huathiri kibofu cha mkojo, mrija wa yurethra na korodani (hutokea kwa nadra), huwa na dalili hizi;
Kuhisi hali ya kuungua kwa kibofu wakati wa kukojoa
Maumivu wakati wa kukojoa
Kutokwa na uchafu uumeni ambao unaweza kuwa na rangi nyeupe, njano au kijani
Maumivu au kuvimba kwa korodani
Gono inayoathiri njia ya haja kubwa
Hutokea sana kwa wanaume wanaoshiriki ngono kinyume na maumbile na wenza wenye maambukizi, huwa na dalili hizi;
Kutokwa na uchafu
Maumivu
Miwasho
Kutoka damu au kupata choo chenye matone ya damu
Maumivu wakati wa kujisaidia
Gono inayoathiri kinywa na koo
Huwapata wanaume wanaofanya ngono ya mdomo na wenza wenye maambukizi.
Mara nyingi maambukizi katika sehemu hii hayaambatani na dalili zozote, hata kama dalili zitaonekana huwa ni vigumu kutofautisha dalili hizo na dalili zingine za magonjwa ya kinywa na koo , na hivyo utambuzi wake huwa mgumu na kuchelewesha matibabu.
Dalili hizi zinaweza kuonekana
Maumivu ya koo
Kuhisi mikwaruzo kwenye koo
Kuhisi koo kukuaka
Koo kuwa jekundu
Homa
Kuvimba kwa mitoki katika shingo
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
3 Desemba 2024, 13:46:21
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. About Gonorrhea. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/gonorrhea/about/index.html. Imechukuliwa 03.12.2024
2. Gonorrhoea (Neisseria gonorrhoeae infection). Health Organization (WHO). https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/gonorrhoea-(neisseria-gonorrhoeae-infection). Imechukuliwa 03.12.2024
3.Gonorrhea: Treatment update for an increasingly resistant organism – PMC. https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC4366410/. Imechukuliwa 03.12.202