top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

27 Machi 2020, 17:48:02

Dalili za magonjwa ya figo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za magonjwa ya figo

Magonjwa ya figo ni mjumuiko wa magonjwa yote yanayoathiri utendaji kazi wa figo. Baadhi ya magonjwa ya figo huweza kwenda mpaka miezi mitatu bila kuleta dalili za kushitukiza kuwa mtu ana tatizo la figo ila mtu huwa na upungufu wa ufanyaji kazi wa figo.


Magonjwa ya figo huweza kuwapata watu wote wake kwa waume na kwa rika zote.


Visababishi


Magonjwa ya figo huweza kusababisha na vitu vifuavyo;


  • Ugonjwa wa kisukari

  • Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu

  • Maambukizi kwenye glumerula

  • Mawe kwenye figo

  • Ugonjwa wa UTI yenye kujirudia rudia

  • Kuziba kwa nefroni

  • Kuziba kwa mirija ya mikojo kama kunakosababishwa na tezi dume au mawe kwenye njia za mkojo

  • Mambukizi kwenye mishipa ya gromerula pamoja na nefroni

  • Sumu, chakula au dawa

  • Ajali /Kuumia eneo la figo

  • Tatizo la kurisi la ugonjwa wa Figo wa polisistiki


Dalili za magonjwa ya figo


  • Uso Kuvimba wakati unaamka asubuh au wakati wote au uvimbe kuzunguka macho

  • Kuvimba kwa miguu

  • Mwili kuvimba mzima

  • Mkojo kutoa povungozi kukauka na kuwasha

  • Uchovu wa mwili na kuishiwa nguvu

  • Kushindwa kuwa makini

  • Kushindwa kupata usingizi

  • Kutokwa damu kwenye mkojo

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Maumivu ya magoti

  • Kuonekana kwa protini kwneye mkojo wa mgonjwa

  • Maumivu ya mwili

  • Kuvimba kiwiko chamkono na magoti

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Uchovu kupita kiasi

  • Maumivu ya kifua kama maji yametuwama kwenye moyo

  • Kuishiwa pumzi kama maji yametuwama kwenye mapafu

  • Shinikizo la juu la damu lililogumu kutibika


Vihatarishi vya kupata magonjwa ya figo


  • Kisukari

  • Shinikizo la juu la damu

  • Uvutaji wa sigara

  • Obeziti

  • Kuwa muafrika

  • Historia ya ugonjwa wkenye familia

  • Figo yenye umbo lisilo la kawaida

  • Umri mkubwa


Namna ya kujikinga na magonjwa ya figo


Fuata maelekezo ya matumizi ya dawa

Unaponunua dawa dukani hakikisha umeandikiwa na daktari na unafuata maelekezo ya namna ya kutumia, dawa kama aspirini, ibrupofen parasetamol(panado) na dawa zenye mchanganyiko wa parasetamo huweza kuharibu figo na kuleta magonjwa ya figo. Kutumia dawa za Maumivu mara kwa mara kunakuweka hatarini kupata magonjwa na yanatakiwa kutotumika kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa figo.


Uzito

Hkikisha unakula vizuri chakula kinachoshauriwa kiafya na kuishi Maisha yanayoshauriwa kiafya

Fanya mazoezi siku 3 hadi 4 za wiki na kazi za kutoa jasho ili mwili uwe imara. Kama una uzito mkubwa ongea na daktari wako kwa ushauri wa namna gani ya kupunguza uzito na uzito gani unakufaa wewe.

Punguza kiasi cha wanga unaotumia ili kuepuka unene.


Usivute sigara na tumbaku

Sigara hudhuru mishipa ya damu ya figo. Kama unavuta sigara ongea na daktari wako namna gani ya utaweza kuacha kuvuta sigara.


Tibu magonjwa yako kwa kupata ushauri kutoka kwa Daktari

Usijitibu mwenyewe bila kupata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wako. Endapo ugonjwa ulionao unaongeza hatari ya kupata magonjwa ya figo basi ongea na daktari wako namna gani ya kuzuia kupata ugonjwa huu.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023, 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Braunwald, E. & Fauci, A.S. (2001). Harrison’s Principles of Internal Medicine. McGraw Hill.

2.Cumming A.D. (2003). Davidson’s Principles and Practice of Medicine. Edinburgh, Oxford: Elsevier Saunders.

3.Kumar, P. & Clark, M. (2007). Clinical Medicine (6th ed.). Edingurgh, Oxford: Elsevier Saunders.

4.National Kidney Foundation. 10. Signs you may have kidney disease. https://www.kidney.org/news/ekidney/august14/10_Signs_You_May_Have_Kidney_Disease Imechukuliwa 27.03.2020
5.Rosenberg M. Overview of the management of chronic kidney disease in adults. http://www.uptodate.com/home. 27.03.2020
6.Coping effectively: A guide for patients and their families. The National Kidney Foundation. https://www.kidney.org/atoz/content/coping_effectively_guide. 27.03.2020

7.Chronic kidney disease: What does it mean for me? National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-communication-programs/nkdep/a-z/kidney-disease-mean-for-me/Pages/default.aspx. 27.03.2020

8.Chronic kidney disease (CKD) and diet: Assessment, management and treatment. National Kidney Disease Education Program. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-communication-programs/nkdep/a-z/Documents/ckd-diet-assess-manage-treat-508.pdf. 27.03.2020

9.Kidney failure: Choosing a treatment that's right for you. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/kidney-disease/kidney-failure-choosing-a-treatment-thats-right-for-you/Pages/facts.aspx. 27.03.2020

bottom of page