Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
29 Machi 2020, 10:16:33
Dalili za mtu aliyekufa
Ni nini maana ya kifo?
Kifo au kufa ni kusimama endelevu kwa kazi zote za kibayolojia mwilini zinazompa kiumbe uhai. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha kifo, ikiwa pamoja na magonjwa na ajali mbaya.
Kitiba kuna aina mbili za kifo, kifo cha sehemu zote za ubongo ikiwa pamoja na shina la ubongo, au kifo cha ubongo kisichohisisha shina la ubongo. Endapo mtu amekufa lakini shina la ubongo bado linafanya kazi mtu mtu huyu mapigo yake ya moyo na upumuaji unaweza endelea. Sehemu hii tumezungumzia kifo kikimaanisha kifo cha ubongo pamoja na shina la ubongo(brainstem)
Dalili mwili uliokufa
Kupotea kwa mapigo ya moyo
Kupotea kwa mapigo ya mishipa ya damu
Kusimama kw aupumuaji
Kutosikika kwa sauti za upumuaji
Kupanuka kwa pupul kusikodhuriwa na mwanga
Kutoonyesha ishara ya maumivu kama yakisababishwa kwenye mwili
Konea kupata ukungu
Mwili kuanza kubadilika ama kuoza
Kushuka kwa joto la mwili- Kuanza kuwa wa baridi kwenye miishio ya mikono na miguu(baadhi ya magonjwa husababisha kupanda kwa joto mara baada ya mtu kufa, joto hili linaweza kukaa masaa kadhaa kabla ya kuanza kushuka)
Mabadiliko yanayotokea mwilini baada ya kufa
Mabadiliko ya ghafla
Mabadiliko ya mapema
Mabadiliko ya muda mrefu
Mabadiliko ya ghafla
Kusimama kwa mfumo wa moyo na mishipa ya damu
Kusimama kwa mfumo wa upumuaji
Kupata mabadiliko kwenye konea ya macho- kuwa na ukungu, kukauka kutochezesha kope na
kupanuka kwa pupil kusiko dhuriwa na mwanga.
Kupotea kwa matendo yasiyohiari ya maungio ya mwili(refleksi)
Kulegea kwa mwili
Mabadiliko ya mapema
Mwili kuwa wa baridi kuanzia kwenye miishio ya miguu na mikono
Kukakamaa kwa misuli na maungio ya mwili
Mwili kubadilika rangi na kuwa kama ya blue ya zambarau
Mabadiliko ya muda mrefu
Mwili kujaa gesi na kuanza kuoza
Mwili kubadilishwa kutoka katika hali ya mafuta na kuwa hali ya kunata (Wax)
Kutuwama kwa maji sehemu ya chini mwili ulipolala- hivyo sehemu hii ya mwili huonekana kama imevimba na kubadilika rangi
Mwili kukauka endapo upo mazingira yaliyo na joto bila kuwa na unyevunyevu
Kufanyika kwa mafuvu- endapo nyama na viungo vingine vyote vimeoza
Kufanyika kwa fosili- fosili ni mifupa ambayo imekaa muda mrefu san ana hivyo huwa na mwonekano wa jiwe.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Bailey FA, et al. Palliative care: The last hours and days of life. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 28.09.2020
2.Institute for Clinical Systems Improvement. Palliative care for adults. Bloomington, Minn: Institute for Clinical Systems Improvement. https://www.guideline.gov/summaries/summary/47629/palliative-care-for-adults. Imechukuliwa 28.09.2020
3.Miller RD. Palliative medicine. In: Miller's Anesthesia. 8th ed. Philadelphia, Pa: Saunders Elsevier; 2015. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.09.2020
4.Survey of Biological Factors Affecting the Determination of the Postmortem Interval pdf. Bautista, Richard. Spring 2012.
5.Michael J. Shkrum, MD etal. Forensic Pathology Trauma. ISBN: 978-1-58829-458-6 page 28,36
6.Burton, J. F. Fallacies in the signs of death. J. Forensic Sci.19:529–534, 1974.
7. Burton, J. F. The estimated time of death. Leg. Med. Annu. 1976:31–35, 1977.
8. Gonzales, T. A., Vance, M., Helpern, M., Umberger, C. J. Legal Medicine, Pathology and Toxicology. 2nd ed. Appleton Century Crofts, New York, 1954.
9. Camps, F. E. Legal Medicine. 2nd ed. John Wright and Sons, Bristol, UK, 1968.
10. Adelson, L. The Pathology of Homicide. Charles C. Thomas, Springfield, IL, 1974.