Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
22 Machi 2020, 22:49:57
Dalili za tezi dume
Tezi dume kwa lugha ya tiba "Prosteti" ni tezi iliyo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume, chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi hii hupitiwa katikati na mrija wa urethra unaotokea kwenye kibofu cha mkojo kwenda kwenye tundu la uume. Mrija huu kazi yake ni kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo.
Kwa kawaida tezi ya prosteti huwa na ujazo na uzito wa gramu 25. Endapo tezi hii itakuwa Zaidi ya ukubwa huu huanza kusababisha dalili mbalimbali kulingana na ukubwa au ujazo.
Tezi ya prosteti hukua kwa jinsi mwanaume anavyoongezeka umri na ifahamike kuwa ni kawaida ukuaji huu kutokea na wala haimaanishi saratani au shida yoyote mwilini.
Dalili za tezi dume huanza kuonekana maranyingi kwenye umri wa miaka 50 na kuendelea kwasababu katika umri huu, tezi huwa imekuwa na hukua zaidi hivyo hupunguza au kuziba kabisa njia ya mkojo. Kukua kwa tezi dume kusikosababishwa na saratani kunaitwa Benaini prostatiki haipaplezia.
Dalili za tezi dume iliyovimba
Kukojoa mkojo wenye mtiririko thaifu
Mkojo kutoka kwa shida wakati wa kuanza kukojoa
Kutumia nguvu ili mkojo utoke wakati wa kojoa
Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
Mkojo kuendelea kutoka kidogokidogo baada ya kumaliza kukojoa au matone ya mkojo kuendelea kutoka
Mkojo kushindwa kutoka hata wakati mtu anapohisi kukojoa
Hisia za kibofu kujaa mkojo wakati wote
Hali ya kujihisi kukojoa mara kwa mara na kwa gafla
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Prostate problems at https://www.niddk.nih.gov/health-information/urologic-diseases/prostate-problems/prostate-enlargement-benign-prostatic-hyperplasia. Imechukuliwa 18.3.2020
2.Benign prostatic hyperplasia at https://www.google.com/url q=https://familydoctor.org/condition/benign-prostatic-hyperplasia. bph/&sa=U&ved=2ahUKEwiOz83JhKToAhWK6aQKHU4VA70QFjARegQIABAB&usg=AOvVaw1aJ-vtnyHPqkRuWDcP1Sqn. Imechukuliwa 18.3.2020
3.Benign prostatic hyperplasia at https://www.google.com/url?q=https://www.urologyhealth.org/urologic-conditions/benign-prostatic-hyperplasia (bph)&sa=U&ved=2ahUKEwiOz83JhKToAhWK6aQKHU4VA70QFjALegQICRAB&usg=AOvVaw2lzVVnDDo4yojVc4FDvbTS . Imechukuliwa 18.3.2020
4.Benign prostatic hyperplasia at https://www.pcf.org/about-prostate-cancer/what-is-prostate-cancer/prostate-gland/what-is-bph/ Imechukuliwa 18.3.2020
5.Prostate enlargement at https://www.google.com/url?q=https://www.webmd.com/men/prostate-enlargement-bph/enlarged-prostate-your-bph-symptoms-score&sa=U&ved=2ahUKEwiOz83JhKToAhWK6aQKHU4VA70QFjAJegQIBhAB&usg=AOvVaw1yKxKHGGmeDB30PcFr-SSn. Imechukuliwa 18.3.2020