Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
26 Machi 2020, 12:39:14
Dalili za ugonjwa wa ini
Ini ni ogani muhimu ndani ya mwili wa binadamu, hupatikana sehemu ya juu kulia ya tumbo. Ini pia huwa chini ya ukuta wa dayaframu, juu ya tumbo, figo ya kulia na utumbo. Kuna kazi nyingi zinazofanywa na Ini, baadhi ya kazi hizo zimeorodheshwa hapa chini.
Kazi ya Ini
Kulinda mwili dhidi ya magonjwa kwa kuondoa bakteria mwilini
Kuhifadhi Vitamini A, D,E,K & B12 na madini chuma
Kushughulika na chakula kilichosagwa kutoka kwenye utombo mdogo
Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mfano fibrinogen, prothrombin
Huharibu na kuondoa sumu na madawa ambayo yanaingia mwilini
Hutengeneza nyongo (bile ) ambayo husaidia kumeng'enya chakula
Kutengeneza vimeng’enya na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi ikiwa pamoja na kuponya tishu zilizoharibika au kuzeeka.
Kuvunjavunja chakula na kutengeneza nguvu inayohitajika mwilini( kuipa mwili nguvu)
Huhifadhi na kutoa sukari inayotoka kwenye chakula ili kutumiaka baadaye
Huvunjavunja kemikali ya hemoglobin
Hurekebisha hali ya damu
Huondoa bilirubini mwilini- kemikali ambayo inaleta manjano.
Aina za magonjwa ya Ini
Magonjwa ya ini yanaweza kuwa yafuatayo;
Magonjwa yanayosababishwa na virusi kama vile homa ya ini inayosababishwa na kirusi cha Hepataitis A,B na C
Magonjwa yanayosababishwa na sumu, dawa au pombe kama vile Ini mafuta na silosisi
Saratani ya ini
Magonjwa ya kurithi kama vile ugonjwa wa hemokromatosisi and ugonjwa wa Wilson
Visababishi vya Magonjwa Ya Ini
Vimelea- kama Virusi vya hepataitiz A, B na C . Kirusi cha hepataitiz B kinaongoza kwa kusababisha ugonjwa wa Ini
Magonjwa ya Autoimyuni
Unywaji wa pombe uliopindukia kwa muda mrefu
Ugonjwa wa ini mafuta
Magonjwa ya Kurithi mfano ugonjwa wa Wilson's
Madawa na sumu zinazoharibu na kudhuru Ini, mfano wa dawa ya parasetamo/panado
Dalili na Ishara za Ugonjwa Wa Ini
Maumivu ya tumbo
Kuvimba kwa tumbo- hii ni kutokana na asaitizi.
Anjano kwenye macho na ngozi, na mkojo
Kutoka damu kwenye fizi au puani bila sababu
Kupata kichefuchefu na Kutapika
Miguu kuvimba
Kupoteza hamu ya chakula na kupungua uzito
Kupumua kwa shida
Kuwashwa mwili kutokana na chumvi ya bile kujikusanya kwenye ngozi
Kupata kaputi medusa (kuonekana kwa mishipa ya damu kwenye tumbo yenye umbo la buibui inayoanzia kwenye kitovu)
Kuhisi kiu sana
Kuhisi Mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi
Mwili kuchoka mara kwa mara
Kupata Kinyesi kilichopauka
Kupata mkojo mweusi
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Stanford children. Anatomy and function of liver. https://www.stanfordchildrens.org/en/topic/default?id=anatomy-and-function-of-the-liver-90-P03069. Imechukuliwa 25.3.2020
2.liver disease at https://www.google.com/url?q=https://www.medicinenet.com/liver_disease/article.htm&sa=U&ved=2ahUKEwixvLDRvbXoAhXErHEKHba1AU8QFjALegQICBAB&usg=AOvVaw10RQ9s_zJlvPSH_bBpoZc8 . Imechukuliwa 25.3.2020
3.liver disease signs, symptoms,causes at https://www.google.com/url q=https://www.emedicinehealth.com/liver/article_em.htm&sa=U&ved=2ahUKEwixvLDRvbXoAhXErHEKHba1AU8QFjAQegQIARAB&usg=AOvVaw0QCb-8wqqCPcARHRVT2Ko4 . Imechukuliwa 25.3.2020
3. Sympotoms of liver disease at https://www.google.com/url q=https://www.urmc.rochester.edu/encyclopedia/content.aspx%3Fcontenttypeid%3D85%26contentid%3Dp00664&sa=U&ved=2ahUKEwixvLDRvbXoAhXErHEKHba1AU8QFjARegQICRAB&usg=AOvVaw0WagVbV2H2dawDbN1xCsqX . Imechukuliwa 25.3.2020
4.liver disease sympotoms at https://www.google.com/url?q=https://www.healthline.com/health/liver-disease symptoms&sa=U&ved=2ahUKEwixvLDRvbXoAhXErHEKHba1AU8QFjAOegQIDhAB&usg=AOvVaw34LoeWUgUrLpxH2xz4OdCH . Imechukuliwa 25.3.2020
5.liver cirrhosis at https://www.google.com/url q=https://www.medicalnewstoday.com/articles/172295&sa=U&ved=2ahUKEwixvLDRvbXoAhXErHEKHba1AU8QFjAMegQIDRAB&usg=AOvVaw37RI_K9mYWsxchNijSvgUr .Imechukuliwa 25.3.2020